WAZIRI KITWANGA AIKANA KAMPUNI YA LUGUMI,AELEZA MAMBO MAZITO
Wakati sakata la Kampuni ya Lugumi kudaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa utambuzi wa vidole kwenye vituo vya polisi likianza kudaliwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema hana uhusiano wowote na kampuni hiyo kama watu wanavyodai.
Kitwanga
ambaye alihusishwa na Lugumi kupitia kampuni ya Infosys iliyodaiwa
kwamba kiongozi huyo ni mmoja wa wanahisa wakati akiwa mfanyakazi wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ameeleza kuwa hahusiki na wala halijui
suala la Lugumi.
Infosys
ambayo imekanusha kuhusika katika sakata hilo imedaiwa kuwa iliisaidia
kampuni ya Lugumi kupata vifaa kutoka kampuni ya Dell ya Marekani ili
viweze kufungwa kwenye vituo vya polisi.
Jana
Kitwanga alisema anashangazwa jinsi anavyohusishwa kwa maelezo kuwa
wakati tukio hilo likitokea mwaka 2011, yeye hakuwa waziri wa wizara
hiyo.
“Inanishangaza
sana sihusiki na wala silijui hili suala la Lugumi. Wakati linatokea
sikuwa waziri wa wizara hii ndiyo maana huwa sipendi na wala sitaki
kuzungumza chochote kuhusu Lugumi,” alisema.
Kitwanga
alifafanua kuwa baadhi ya mambo yameanza kubainika baada ya kuteuliwa
kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, licha ya kutotaka kuweka wazi
kama suala la Lugumi ni miongoni mwa mambo hayo.
Kampuni
ya Lugumi ilibainika kutotimiza matakwa ya mkataba wake baada ya
kufunga mashine 14 tu kati ya 108 zilizotakiwa kufungwa, licha ya
kulipwa zaidi ya asilimia 90 ya fedha kwa mujibu wa mkataba.
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14 ndiyo iliyofichua udhaifu huo.
Utekelezwaji
wa mkataba huyo uliwasilishwa jana kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC) na mwenyekiti wake Aeshi Hilaly alisema wameanza kuupitia
na watakapokamilisha wataweka kila kitu wazi.
Kwa upande wake Ndugai alipotakiwa kuzungumzia suala hilo alisema, “Mimi sijapata taarifa zozote za Lugumi. Jambo hilo bado lipo katika kamati ya bunge.
WAZIRI KITWANGA AIKANA KAMPUNI YA LUGUMI,AELEZA MAMBO MAZITO
Reviewed by The Choice
on
2:52:00 PM
Rating:

No comments: