VIDEO YA NDI NDI NDI KUMRUDISHA LADY JAY DEE KWA JUSTIN CAMPOS
Baada
ya miaka 10 ya kufanyakazi na muongozaji wa video Justin Campos,
Komando Jide au Lady Jaydee amerudi tena kwake kufanyanaye kazi,
kutengeneza video ya wimbo wake wa #NdiNdiNdi
Taarifa
hiyo ya kufanyakazi na Justin Campos ameitoa Lady Jaydee mwenyewe
kwenye ukurasa wake wa Instagram, baada ya kupost video ikimuonyesha
Justin Campos akisema ni heshima kwake kufanyakazi na Jaydee ingawa si
mara ya kwanza.
“Nilikutana
na Justin Campos kwa mara ya kwanza 2006 wakati tunafanya video ya
'Njalo' nilioshirikiana na kundi la Afrika Kusini linalojulikana kama
'Mina Nawe', Justin ndio alikuwa Director wa video hiyo baada ya miaka
10 tumefanyanae kazi tena 2016,” aliandika Jaydee.
Pia
Lady Jaydee ameanza kupost picha za video hiyo huku akiandika
“#NdiNdiNdi loading Kikomandooooooo #NguvuYaUmma #WananchiWameipokea
#NdiNdiNdiMusicVideo”.
Alichokiandika Jaydee kuhusu video ya NdiNdiNdi
VIDEO YA NDI NDI NDI KUMRUDISHA LADY JAY DEE KWA JUSTIN CAMPOS
Reviewed by The Choice
on
9:37:00 AM
Rating:
No comments: