NYOTA WA KIKAPU KOBE BRYANT ASTAAFU KUCHEZA KIKAPU NA LEO NDIO GAME YAKE YA MWISHO
Mcheza
kikapu nyota wa Los Angeles Lakers Kobe Bryant anatarajia kustaafu
kuichezea Ligi ya NBA leo siku ya Jumatano 13 April 2016.
Kobe
mwenye miaka 37 atacheza mechi yake ya mwisho kwenye NBA dhidi ya
Lakers na Utah Jazz katika Uwanja wa Staples Center jijini Los Angeles,
California.
Kobe amewahi kuwa bingwa wa All Star mara tano na amecheza NBA All Star mara 18 kwenye maisha yake ya NBA.
Kobe
Bryant amefunga pointi 33,570 katika maisha yake ya uchezaji mpira wa
kikapu (miaka 20) katika historia ya NBA, na kumfanya kuwa mcheza kikapu
wa tatu katika historia ya NBA.
Kobe Bryant ameichezea LA Lakers kwa miaka yote hiyo ambapo alisajiliwa mwaka 1996.
NYOTA WA KIKAPU KOBE BRYANT ASTAAFU KUCHEZA KIKAPU NA LEO NDIO GAME YAKE YA MWISHO
Reviewed by The Choice
on
6:53:00 AM
Rating:
No comments: