MWANAUME MWENYE WAPENZI 17 AZUA MTAFARUKU HOSPITALI
Waandishi nao walikuwepo kushuhudia kituko hicho cha karne alichosababisha bwana Yuan.
Mwanamume mmoja raia wa
Chini anaendelea kupata ahueni baada ya kupata ajali ya gari ,lakini
akajikuta katika wakati mgumu baada ,wakati mabibi zake wote kumi na
saba walipoamua kwenda kumjulia hali katika hospitali alikolazwa.
Shababi huyo anaitwa Yuan,
anayetokea Changsha,alipatwa na ajali ya gari mwezi March 24 na amelazwa
hospitalini tangu wakati huo.wanawake hao hawakuwahi kujua kuwa bwana
Yuan ana idadi hiyo ya wanawake,na hakuna aliyedhani kuna
aliyemzidi,mmoja wao aliishi na Yuan kwa muda wa miaka tisa na kujaaliwa
mtoto mmoja wa kiume,na bado hakutanabahi kuwa wako wengine kumi na
sita nyuma yake.
Mwanamke huyo aling’amua
siri ya laazizi wake baada ya madaktari kuwapigia simu wanawake wote
kuwataarifu kuwa bwana wao ameumia ajalini.
Bibi mmoja aitwaye Xiao Li,
alikuwa akijiachia kimahaba na shababi Yuan kwa miezi kumi na nane
amesema kwamba nilipatwa na mashaka makubwa baada ya kutaarifiwa mkasa
uliomfika,lakini nilistaajabishwa na idadi ya warembo waliokuwa
wakiingia kila dakika kumjulia hali,niliacha kulia papo hapo .
Mrembo mwingine aliropokwa kwamba haelewi ingekuwaje mbeleni,kwani alishaanza mipango ya harusi na bwana Yuan.
Wang Fang, mama mwenye
mtoto wa kiume aliyezaa na Yuan,amevurugwa na hali ya bwana huyo kiasi
cha kujiuliza maswali yasiyo na majibu kuwa afanye nini sasa, akajikuta
akisema hampendi Yuan tena lakini anampenda mtoto wake wa kiume.Uso wa Yuan ulikua mdogo, baada ya siri yake kubumburuka.
Wanawake hao wakaona isiwe taabu wamefungua kijikundi chao katika
Facebook,kwa lengo la kufungua mdahalo wa majadiliano juu ya kisanga
chao hicho,na pia kutaka kujua walivyochezewa shere na shababi huyo.
Habari hii imezusha gumzo katika mitandao ya kijamii,walio wengi
wakimlaumu mwanamume huyo kwa kitendo chake na wengine walivutiwa na
uwezo wake wa kucheza na wanawake kumi na saba kwa wakati mmoja.
Kutokana na hali hiyo Polisi nchini China wameanzisha uchunguzi
kuhusiana na madai ya udanganyifu alioufanya bwana Yuan,na ni mapema mno
kuzungumzia lolote juu ya mabibi wa bwana huyo kuwa ni waathirika wa
kashfa ya kimapenzi
MWANAUME MWENYE WAPENZI 17 AZUA MTAFARUKU HOSPITALI
Reviewed by The Choice
on
7:58:00 AM
Rating:
No comments: