Mtu mmoja avamiwa na kukatwa miguu yote Morogoro


Watu hao wanadaiwa kumshambulia kwa shoka na panga na kumtelekeza katika mashamba ya miwa.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa akiwa amelazwa katika hospitali ya mtakatifu Francis ya mjini Ifakara majeruhi wa tukio hilo bakari ameeleza namna ambavyo alikumbwa na mkasa huo wakati akitoka kumsindikiza rafiki yake aliyejulikana kwa jina moja la Hamza ndipo alishambuliwa na watu hao.

Nao ndugu wa majeruhi huyo akiwemo mkewe Basilisa Sprian wameeleza kusikitishwa na kitendo kibaya alichofanyiwa ndugu yao huku wakiomba msaada wa hali na mali utakaosaidia kuyanusuru maisha ya kijana huyo.

Kwa upande wake mganga wa zamu wa hospitali hiyo amekiri kumpokea majeruhi huyo akiwa katika hali mbaya huku kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwatukio hilo ambapo amesema jehi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Mtu mmoja avamiwa na kukatwa miguu yote Morogoro Mtu mmoja avamiwa na kukatwa miguu yote Morogoro Reviewed by The Choice on 8:01:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.