MSANII MZEE YUSSUF ADAI WAKE ZAKE WANANIVURUGA AKILI
Mkurugenzi
wa Kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yussuf amesema hakuna kitu
kinamuumiza kichwa kama kutoelewana kwa wake zake wawili.
Akizungumza
katika kipindi cha Sporah Show cha Clouds TV, Mzee Yussuf amesema
anapitia wakati mgumu sana kuwamiliki wake wawili anaowapenda wakati wao
hawapendani.
“Kusema
kweli napata wakati mgumu kuwahandle, yanii linanivuruga sana hili
swala,” alisema Mzee Yussuf. “Ndio maana natamani hata kesho waelewane.
Sometime ni raha wakiwa hawaelewani kwa maana hata kama nimeenda pahali
labda nimezunguka hakuna anayelinda” alifafanua zaidi.
“Lakini
hii ni chugu sana, hili kwangu ni tatizo, natakamani leo au kesho
waelewane. Lakini tatizo la hawa yote ni watu wa karibu, ndio maana mimi
nimeshawaambia kwa mdomo wangu, hili jambo nataka liishe, sitaki kusema
naomba liishe kwa sababu nilishawaomba sana, na ninachoona ustaa ndio
unawasumbua wanashindwa kujua mimi ni staa zaidi yao,” aliongeza Mzee
Yussuf.
Mwanzo
wa mwaka huu, Mzee Yussuf alidai wake zake Leila Rashid na Chiku
awamekatazwa kutumia mtandao wa Instagram kwa madai mtandao huo unakuza
ugomvi wao.
Bongo 5
MSANII MZEE YUSSUF ADAI WAKE ZAKE WANANIVURUGA AKILI
Reviewed by The Choice
on
6:32:00 AM
Rating:
No comments: