MSANII CYRIL AMGONGA TRAFIKI NA KUMJERUHI VIBAYA
Msanii wa Bongo Fleva, Cyril Kamikaze aliyedaiwa kumgonga trafiki.
Msanii
wa Bongo Fleva, Cyril Kamikaze yamemkuta baada ya kuswekwa nyuma ya
nondo za mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar, kufuatia
msala wa kudaiwa kumgonga na kumburuza kwa gari trafiki aliyemsimamisha
barabarani, aliyejitambulisha kwa jina la Afande Francis.
Kwa
mujibu wa chanzo cha kuaminika ambacho ni mmoja wa mashuhuda, tukio
hilo lililokuwa kama sinema ya kivita lilijiri wiki iliyopita majira ya
saa 5:00 asubuhi jirani na Hospitali ya Magomeni, Dar, wakati trafiki
huyo akitekeleza majukumu yake ya kuongoza magari barabarani.
Ilidaiwa kuwa, trafiki huyo alimsimamisha Cyril ambaye alimpuuza na kumgonga.
“Alichokifanya Cyril ni unyama, kama alijijua ana makosa angesimama tu na kumsikiliza.
Afande Francis anayedaiwa kugonga na Cyril na kusababishiwa majeraha.
“Kwanza
alimgonga, yule trafiki akajihami kwa kurukia juu ya gari kwa mbele
(kwenye boneti), akazidi kukimbiza gari ili ammwage barabarani.
“Hata
hivyo, mashuhuda walimsifu sana yule trafiki maana kama asingekuwa yupo
fiti kwa kujiokoa, basi angekufa,” kilisema chanzo hicho.
Kwa
upande wake trafiki huyo alipoombwa na Ijumaa Wikienda kuelezea mkasa
huo, huku akiwa na masikitiko makubwa alisema, hadi sasa haamini kama
yupo hai kutokana na ujasiri mkubwa alioutumia kujiokoa, kwa kuwa kila
anapojiuliza Cyril alikusudia nini, anakosa jibu.
“Niliona
gari ndogo lenye ‘tinted’ nzito linakuja, nikaamua kulisimamisha, cha
ajabu likasimama lakini baada ya kuona nakaribia kulifikia akaliondoa
kwa kasi na kunigonga. Ndipo nikachukua bodaboda kulikimbiza hadi kwenye
Kona ya Kwa-Shehe Yahya.
.Baadhi ya majeraha madogo aliyoyapata afande huyo.
“Pale
pia hakusimama, akavuka upande wa pili, kulikuwa na gari la driving
school, nikaliamuru ‘lim-block’. Nikashuka kwenye bodaboda na kusimama
mbele ya gari lake.
“Badala ashuke, ndiyo kwanza akalitoa gari kwa kasi huku akiniburuza na kunigonga,” alisema Afande Francis.
Alisema baada ya kuona hivyo,
alilazimika kujirusha kwenye boneti ya gari hilo ili kunusuru uhai wake,
lakini Cyril hakujali kwani aliendelea kuendesha kwa kasi akiliyumbisha
ili afande huyo aishiwe nguvu na kuanguka barabarani.
Gari lake likiwa chini ya ulinzi.
“Lengo
lake lilikuwa animwage kisha anikanyage na gari ili nife, alipoona
nimeshikilia wepa, akawa anazichezesha nikose pa kushika, ikanilazimu
nipige ngumi kioo cha gari, mkono ukapita ndani nikamshika ndo
akasimamisha gari.
Alikuwa akikimbia kwa sababu gari lake limekutwa vibali vimeisha na hakuwa na leseni,” aliongeza Afande Francis.
Kufuatia ishu hiyo, trafiki huyo
anaendelea vizuri japokuwa ana majeraha madogo mkononi huku msanii huyo
akishikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Magomeni kwa jalada la
kesi namba MAG/TR/RB/110/206 SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI NA KUKATAA AMRI
HALALI 13/4/2016 akisubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa msala
huo ambao umemkalia vibaya.
MSANII CYRIL AMGONGA TRAFIKI NA KUMJERUHI VIBAYA
Reviewed by The Choice
on
9:37:00 PM
Rating:
No comments: