MENEJA BABU TALE ASEMA KOLABO YA MADEE NA TEKNO IMEKAMILIKA
Meneja
wa Tip Top Connection, Babu Tale amesema msanii wake Madee tayari ana
ngoma 6 mpya ambazo hazitatoka, ambapo moja kati ya hizo ni kolabo yake
na Tekno.
Akizungumza
katika kipindi cha The Playlist cha Times FM, Babu Tale amesema
anasubiria wakati ufike aanze kuachia kazi hizo ambazo amedai ni kali.
“Nina
nyimbo sita mpya za Madee zinanichanganya,” alisema Tale. “Kuna wimbo
kafanya na Tekno, kuna ngoma tatu ameshafanya na video. Kuna ngoma
tunafanya video Jumatatu, nachanganyikiwa sijui nifanyeje kwa sababu
nina ngoma kali za Madee”,
Aliongeza,
“Wakati Madee anarudi kila mmoja ataongea kama nambeba, lakini Madee
kila mtu anajua ana mwaka mmoja hajaachia ngoma”,
CHANZO na Bongo5
MENEJA BABU TALE ASEMA KOLABO YA MADEE NA TEKNO IMEKAMILIKA
Reviewed by The Choice
on
7:15:00 AM
Rating:
No comments: