Maneno ya Le Mutuz baada ya Mama yake ‘Anne Kilango Malecela’ Kutumbuliwa JIPU kwenye ukuu wa mkoa na RAIS MAGUFULI
Jina lake la kuzaliwa ni William Malecela na jina lake maarufu la mitandaoni ni Le Mutuz ambaye ni mmiliki wa williammalecela.com na jana April 11 2016 aliamua
kuwajibu wanaomuandama kutokana na uteuzi wa ukuu wa mkoa wa Shinyanga
chini ya Anne Kilango Malecela ambaye ni mama yake kutenguliwa.
Le Mutuz Aliandika:
"Guys naomba kusema hivi nimepigania Rais Magufuli kuwa Rais na
ninamuunga mkono kwa juhudi zake za kusafisha uozo hata kama unamuhusu
Mama yangu mzazi kwa sababu hata mimi wafanyakazi wa Kampuni yangu
wasipofuata masharti yangu kama muajiri ni lazima niwaondoe sasa Nina
wafanyakazi 4 ambao ili kuwa nao nilipitia kama watu 100
"Now
nimesikia kwamba Mama yangu hakufuata masharti ya muajiri wake so
amefukuzwa kazi kwangu sina pingamizi wala ishu na Rais kwa sababu
Sheria ni msumeno inatakiwa kukata kote….now naona maneno mengi sana
ambayo hayana UKWELI wala Msingi ndani yake
"Nimekaa
Majuu Miaka 30 nimerudi Bongo nimesota nimeanzisha Kampuni yangu ya
BLOGU YA WANANCHI MEDIA COMPANY LTD na sasa hivi nipo njiani kuhamia
kwenye RADIO na TV now katika Maisha yangu sijawahi kuishi kwa
kumtegemea mtu ila ninaishi kwa kumtegemea MUNGU‘
"Nilikuwa
nafagia Majuu na pia nahangaika Baharini wakati Baba yangu Makamu wa
Rais na Waziri Mkuu Leo eti Maisha yangu yataharibika kwa sababu Mama
yangu sio RC? hahahaha imenichekesha sana hizi CHUKI guys zitawaua bure
mnazitoa wapi? ….I mean Jana nimerudi Nairobi na sasa najitayarisha
kwenda South Africa weekend hii na nikirudi ni safari ya Dubai eti Mama
yangu kuwa RC wa Wiki Mbili Shinyanga kunahusika na Maisha yangu hapa
Mjini Downtown na hizi Safari zangu za kikazi?
"Hahahahahaha
imenichekesha sana guys nimeshasema Mara nyingi kwamba ninajua sana
kwamba uhusiano wa Public na Watu Maarufu huwa ni feki ila sikutegemea
kwamba watu wanaweza kuwa na CHUKI za mpaka kulazimisha kwamba eti u RC
wa Mama yangu kwa Wiki Mbili tu unahusika na Maisha yangu hapa Downtown
kwamba Nina Ofisi
"Apartment
na Kampuni kwa sababu Mama yangu alikuwa RC wa Shinyanga kwa Wiki Mbili
tu na sasa Maisha yangu yataisha HAHAHAHAHAH jamani this is the best
joke of my life….otherwise guys nimewasikieni ila ninasimama na Rais
Magufuli na I feel sorry for my Mum ila ni Kawaida in life na Sheria ni
msumeno ….otherwise Lov U guys HAHAHAHAHa and I am Super Humbled U know"
– le Mutuz Nation
Maneno ya Le Mutuz baada ya Mama yake ‘Anne Kilango Malecela’ Kutumbuliwa JIPU kwenye ukuu wa mkoa na RAIS MAGUFULI
Reviewed by The Choice
on
7:07:00 AM
Rating:
No comments: