Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Yatahadharisha Mvua Kubwa za Upepo Mkali
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa inayozidi milimita 50 wiki hii.
Imesema
mvua hizo ambazo zitanyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga,
Pwani, Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba zitakuwa kubwa na
kuweza kusababisha madhara.
Taarifa
iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi ilisema mvua
hizo zilitarajia kunyesha kuanzia Aprili 13, mwaka huu hadi Jumamosi
Aprili 16, mwaka huu.
Dk
Kijazi alisema kiwango cha uhakika wa mvua hizo ni kwa asilimia 70 na
hali hiyo imetokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua sambamba na uwepo wa
kimbunga cha Fantala katika Bahari ya Hindi.
Hivyo
aliwataka wananchi wanaokaa maeneo yaliyotajwa kuchukua hadhari na
kuchukua hatua stahili ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza
kutokana na mvua hizo kubwa.
Hivi
karibuni, TMA ilisema mvua za masika katika ukanda wa Pwani zilizoanza
wiki ya kwanza ya mwezi huu kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa
zitakazoweza kusababisha mafuriko.
Aidha, kwa wakati huo hali ya joto kali itaendelea kuwepo nyakati za usiku huku ikipungua nyakati za mchana.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Yatahadharisha Mvua Kubwa za Upepo Mkali
Reviewed by The Choice
on
7:20:00 AM
Rating:
No comments: