Halima Mdee Amtaka Rais Magufuli Ataje Posho na Marupurupu Anayolipwa Yote
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee
amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata
ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.
Mdee
ambaye ni mbunge wa Kawe, alitoa ombi hilo jana kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi,
uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo.
Kauli hiyo ya
Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa
ni Sh9.5 milioni kwa mwezi.
“Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5
milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi
ambacho anakipata,” alisema Mdee.
Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.
“Sisi
wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni,
lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10
milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,” alisema Mdee.
Mbunge
wa Jimbo la Ndanda katika Wilaya ya Masasi, Cecil Mwambe alidai katika
mkutano huo kuwa wananchi wa Mtama wamekosa mwakilishi wa kuwasemea
matatizo yao, hasa ya upande wa kilimo cha korosho kutokana na mbunge
wao, Nape Nnauye kukosa uwezo wa kusimama bungeni kuisema Serikali.
Halima Mdee Amtaka Rais Magufuli Ataje Posho na Marupurupu Anayolipwa Yote
Reviewed by The Choice
on
8:19:00 AM
Rating:
No comments: