HAJI MANARA ANUSURIKA KIFO KWENYE AJALI MBAYA YA BARABARANI
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Haji Manara amepata ajali mbaya.
Manara amepata ajali baada ya kuchomoka tokea ndani ya Bajaj na kuanguka barabarani.
Kuanguka
huko kumesababisha Manara kupata majeraha sehemu za mkononi na usoni
hukua kisema amenusurika kifo kutokana na ajali hiyo.
Manara ameelezea tukio hilo:
“Nilikuwa
nakwenda kumuona shangazi yangu, nikaamua kuacha gari nichukue Bajaj.
Sasa tukio hilo limetokea hivi; Bajaj ilipiga tuta wakati nikiwa
sijashika, ndiyo nikachomoka.
“Hakika
nimeumia na nina maumivu makubwa sana, lakini namshukuru Mungu kwa kuwa
ilikuwa ni ajali mbaya sana hasa kama kungekuwa na gari nyuma.”
HAJI MANARA ANUSURIKA KIFO KWENYE AJALI MBAYA YA BARABARANI
Reviewed by The Choice
on
6:35:00 AM
Rating:
No comments: