WAZIRI MKUU ATUA SIMIYU .. KUTUMBUA MAJIPU KWA WATENDAJI WABOVU
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kutafutwa kwa Ofisa Ardhi
wilayani Busega aliyetoa hati na kibali cha kumuuzia Mtanzania mmoja
mwenye asili ya Asia majengo yaliyokuwa yakitumiwa kwa ujenzi wa
barabara ambayo yaligeuzwa shule.
Katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu,
Waziri Mkuu ameanza kusaka majipu kwa kuagiza kusakwa kwa mtumishi huyo
wa umma.
Kwa mujibu wa Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni, majengo hayo
yaliyokuwa yakitumiwa na kampuni ya ujenzi ya SK Investment Company
Limited, yamebadilishwa hati na kuuzwa kinyemela kwa mtu aliyemtaja kuwa
ni Mtanzania mwenye asili ya Asia.
Dk Chegeni alisema majengo hayo yalikuwa yakitumika na yanaendelea kutumika kama shule ya sekondari.
Akizungumzia sakata hilo, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kusakwa kwa
ofisa huyo ili aeleze kwa nini alitoa kibali na hati hiyo kinyume cha
taratibu.
WAZIRI MKUU ATUA SIMIYU .. KUTUMBUA MAJIPU KWA WATENDAJI WABOVU
Reviewed by The Choice
on
8:51:00 AM
Rating:

No comments: