Walinzi Watatu wa Suma JKT Watiwa Mbaroni Kwa Wizi wa Kompyuta 50 Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM )
Walinzi
watatu wa Suma JKT na askari mmoja wa Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa
Dodoma, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa kompyuta zinazokadiriwa
kufikia 50 mali ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom).
Chanzo
chetu cha habari kilieleza kuwa wizi huo ulitokea juzi baada ya chuo
hicho kufungwa kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka.
Inadaiwa
kuwa katika wizi huo baadhi ya walinzi wa Suma JKT ambao wanajukumu la
kulinda chuo hicho, walihusika huku watatu wakishikiliwa na polisi.
Hata
hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa baadhi ya askari wa Kituo Kikuu cha
Polisi Dodoma wanadaiwa kuhusika na kuzua mkanganyiko katika uchunguzi
wa tukio hilo.
“Katika
wizi huo, pia kuna askari kutoka mjini ametajwa na walinzi wa Suma JKT
kuhusika, sasa baada ya kupata taarifa hizo ndiyo wanafanya mpango wa
kumkamata,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Ofisa
Habari wa Udom, Beatrice Baltazar jana alithibitisha kuwapo kwa tukio
hilo na kwamba, bado hawajajua idadi kamili ya kompyuta zilizoibiwa.
“Ni
kweli kuna wizi wa kompyuta hapa chuoni, lakini sijajua idadi kamili ya
kompyuta zilizoibwa, ila kuna walinzi watatu wa Suma JKT wanashikiliwa
na polisi kwa mahojiano,” alisema Beatrice.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa naye alithibitisha kuwapo
kwa taarifa za tukio hilo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani
kwa kuwa yupo likizo.
Hata hivyo, Mambosasa alikanusha kuwa hakuna polisi aliyehusika katika tukio hilo bali ni walinzi wa Suma JKT.
Walinzi Watatu wa Suma JKT Watiwa Mbaroni Kwa Wizi wa Kompyuta 50 Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM )
Reviewed by The Choice
on
12:10:00 PM
Rating:
No comments: