Trump asema asipochaguliwa huenda fujo zikazuka Marekani
Mfanyabiashara
tajiri Marekani Donald Trump, amesema anafikiri kutatokea fujo iwapo
ataongoza kwa wajumbe kisha chama chake cha Republican kitakosa
kumuidhinisha awanie urais.
Bw Trump alishinda mchujo katika
majimbo matatu zaidi, likiwemo jimbo la Florida mnamo Jumanne, ingawa
alishindwa katika jimbo jingine muhimu la Ohio.Hatua yake ya kushindwa Ohio huenda ikawawezesha wahafidhina wadhibiti wa chama cha Republican, ambao hawajafurahishwa na mtazamo wake, kumpendekeza mgombea mwingine kwenye mkutano mkuu wa kuidhinisha wagombea Julai.
Katika chama cha Democratic, Hillary Clinton ameimarisha uongozi wake na kumshinda mpinzani wake wa pekee Bernie Sanders katika majimbo manne yaliyofanya mchujo Jumanne.
Trump asema asipochaguliwa huenda fujo zikazuka Marekani
Reviewed by The Choice
on
8:15:00 PM
Rating:
No comments: