TRA WAMTAKA PROFESA TIBAIJUKA KULIPA KIASI CHA SH. MILIONI 500 KUTOKA KATOKA MGAWA WA ESCROW
Hatima ya kesi ya Mbunge wa
Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka kupinga kuilipa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) zaidi ya Sh500 milioni kutoka katika mgawo wa Sh1.62
bilioni zinazohusishwa na fedha zilizochotwa Akaunti ya Tegeta Escrow,
itajulikana Machi 29, wakati Bodi ya Rufaa za Kodi (Trab) itakapotoa
uamuzi.
Tarehe hiyo imepangwa na
Makamu Mwenyekiti wa Trab, Hakimu Agusta Mmbando baada ya kukamilika kwa
hatua ya usikilizwaji pande zote mbili kwenye kesi hiyo.
Profesa Tibaijuka alikata
rufaa Trab baada ya TRA kumpelekea madai ya malipo ya kodi ya Sh586
milioni kutokana na mgawo wa Sh1.62 bilioni anazodaiwa kupokea kutokana
na fedha zilizochotwa kutoka akaunti hiyo iliyofunguliwa na Shirika la
Umeme (Tanesco) na kampuni ya kufua nishati hiyo ya IPTL kwa ajili ya
kuhifadhi fedha za malipo ya ununuzi wa umeme wakati mzozo wao ukiwa
mahakamani, lakini zikachotwa kwa njia ambayo ilizua shaka. Rufaa hiyo
ilisikilizwa na Hakimu Mmbando Februari 17, 19 na 22 wakati Profesa
Tibaijuka alipokuwa akitoa ushahidi.
Inadaiwa kuwa Profesa
Tibaijuka, ambaye aliondolewa katika wadhifa wake wa Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokana na sakata hilo, aliwekewa fedha
hizo kwenye akaunti yake na James Rugemalira, Mkurugenzi wa VIP
Engineering & Marketing Limited iliyokuwa kati ya wanahisa wa IPTL.
Kutokana na mgawo huo,
Desemba 31, 2015, TRA ilimtaka alipe kodi hiyo, baada ya kushindwa
kufanya marejesho kutokana na mgawo huo.
Hata hivyo, alipinga madai
hayo na kisha akakata rufaa Trab kupinga hatua ya TRA kumtaka alipe
kiasi hicho cha kodi, pamoja na mambo mengine akidai kuwa hajawahi
kupokea fedha hizo kutoka kwa Rugemalira.
Katika rufaa hiyo namba 22
ya mwaka 2015, Profesa Tibaijuka anadai kuwa makadirio hayo ya TRA ya
malipo ya kodi ni kinyume cha Sheria ya Kodi na hakupaswa kufanya
marejesho kwa kuwa hakupokea kipato chochote katika muda huo uliotajwa.
Akiongozwa na wakili wake,
Dk Nshalla Rugemeleza wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, Profesa
Tibaijuka alidai kuwa fedha hizo zilikuwa ni mchango uliotolewa kwa
Taasisi ya Joha Trust, kwa ajili ya Shule ya Wasichana ya Barbro
Johansson inayomilikiwa na taasisi hiyo.
Profesa Tibaijuka alidai
kuwa yeye si mwanahisa wa taasisi hiyo, bali ni mmoja wa wadhamini na
kwamba TRA ilipuuza ushahidi wake kuwa VIP ilitoa mchango kwa Joha Trust
na yeye kama mdhamini alizipeleka Joha Trust kupitia Bank M.
Aliongeza kuwa TRA
haikuzingatia ukweli kwamba Joha Trust na yeye ni vitu viwili tofauti,
huku akisisitiza kwamba fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya Joha.
TRA WAMTAKA PROFESA TIBAIJUKA KULIPA KIASI CHA SH. MILIONI 500 KUTOKA KATOKA MGAWA WA ESCROW
Reviewed by The Choice
on
9:34:00 PM
Rating:
No comments: