POLISI WAFYATUA MABOMU YA MACHOZI MBELE YA BENKI YA CRDB, TAWI LA MBAGALA-RANGI TATU, NI KUFUATIA UBISHI WA WATEJA KUTUMIASIMU NDANI YA BENKI

POLISI wamelazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliojikusanya mbele
ya
Benki ya CRDB tawi la Mbagala-Rangi Tatu, baada ya mtu mmoja
aliyekuwa akiongea na simu ndani ya benki hiyo kukaidi maagizo ya polisi
ya kuacha kufanya hivyo mapema leo mchana Machi 11, 2016.
Kwa mujibu
wa watu walioshuhudia tukio hilo, watu watatu mmoja akiongea na simu
na wengine wawili waki-chat, ndani ya benki hiyo, waliagizwa na mlinzi
wa benki kuacha kufanya hivyo lakini wakakaidi.
Baada ya
mlinzi kuona hivyo alitoa taarifa kituo cha polisi Mbagala-Maturubai,
na ndipo polisi wakiwa ndani ya gari lao maarufu kama Defender,
waliwasili kwenye eneo hilo na kuamuru watu hao ambao wanaelezwa kuwa
wateja, kutoka ndani ya benki hiyo.
Hata hivyo palitokea mabishano baada ya mmoja wao kukaidi amri ya polisi na kuanza
kupigana nao.
kupigana nao.
Kuona hivyo
watu walianza kujaa na polisi bila kufanya ajizi wakafyatua mabomu
ya machozi kutawanya watu na kuwadhibiti “wateja’hao wabishi na
hatimaye kufanikiwa kuondoka nao.
Hali hiyo ilizua tafrani hadi watu wakadhani kuwa palikuwepo na tukio la ujambazi kwani
ni mwezi uliopita umbali wa mita chache kutoka kwenye benki
hiyo, palitokea tukio baya la uvamizi wa benki ya Access ambapo watu
kadhaa waliauawa wakiwemo polisi.
POLISI WAFYATUA MABOMU YA MACHOZI MBELE YA BENKI YA CRDB, TAWI LA MBAGALA-RANGI TATU, NI KUFUATIA UBISHI WA WATEJA KUTUMIASIMU NDANI YA BENKI
Reviewed by The Choice
on
11:24:00 PM
Rating:

No comments: