Polisi Afukuzwa Kazi Kwa Kutorosha Mtuhumiwa
Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limemfukuza kazi askari wake kwa kudaiwa
kumtorosha mtuhumiwa wa mauaji katika kituo cha Luguru wilayani Itilima,
mkoani hapa.
Pia, linawashikila askari saba wanaodaiwa kuwatorosha
watuhumiwa wengine watatu wa mauaji na ujangili wilayani Meatu kwa
uchunguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
jana, Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Onesmo Lyanga alisema askari huyo
amefukuzwa kazi kwa kulifedhehesha jeshi na atafikishwa mahakamani
kujibu tuhuma hizo.
“Februali 2, mwaka huu katika Kituo cha Polisi
Lugulu, askari alimtorosha mtuhumiwa wa kesi ya mauaji Itl/Ir/95/2016,
mkazi wa Kijiji cha Gambasingu wilayani Itilima,” alida Kamanda Lyanga.
Hata
hivyo, alisema polisi wanaendelea kuchunguza tukio la kutoroka kwa
watuhumiwa wa ujangili wilayani Meatu, na linaendelea kuwashikilia askari
wengine saba.
Alisema tukio hilo lilitokea Januari 19, 2016,
usiku katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Meatu mkoani hapa na kusababisha
watuhumiwa hao kutoboa ukuta na kutoka.
Kamanda huyo aliwataja
watuhumiwa waliotoroka kuwa ni mkazi wa kijiji cha Mwasungula aliyekuwa
akikabiliwa na kesi ya mauaji na wengine wawili ni wakazi wa kijiji cha
Sapa wanaotuhumiwa kukutwa na pembe za tembo.
“Watuhumiwa
waliotoroka katika mahabusu siyo ambao walihusika kutungua helkopita na
kusababisha mauaji ya rubani Rogers Gower, raia wa Uingereza kama baadhi
ya vyombo vya habari vilivyo ripoti, watuhumiwa hao wapo,”alisema Lyanga.
Polisi Afukuzwa Kazi Kwa Kutorosha Mtuhumiwa
Reviewed by The Choice
on
8:26:00 AM
Rating:
No comments: