MSANII HARMONIZE ASEMA HAYA KUHUSIANA NA 'BEEF' LA DIAMOND NA ALI KIBA
Msanii
wa bongo fleva,Harmonize ambaye yuko chini ya lebel ya wasafi
inayomilikiwa na Diamond amefunguka na kusema yeye hajui kama kuna
ugomvi wowote kati ya bosi wake na Ali Kiba kwani hajawai kusikia
akimzungumzia vibaya msanii huyo.
Harmonize
pia ameenda mbali na kusema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Ali Kiba
kama itatokea kwani ni moja kati ya msanii mkali.
“Mimi
sijui kama kuna beef,sijawahi kumsikia Diamond akimwongelea msanii
yeyote tofauti..Diamond ni kati ya watu wanao support muziki wa
Tanzania,ukiona kolabo nyingi za wasanii wa Tanzania na nje Diamond ana
Mchango wake” na kuendele kusema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Kiba “Ali Kiba ni msanii mzuri,kwa hiyo kolabo ikiwa na tija nitafanya naye“.
Source: CloudsTv
MSANII HARMONIZE ASEMA HAYA KUHUSIANA NA 'BEEF' LA DIAMOND NA ALI KIBA
Reviewed by The Choice
on
6:46:00 AM
Rating:
No comments: