MASKINI WEEEE : Yabainika Rashford kanyimwa gari la bure klabuni
MASKINI wa leo ndiye tajiri wa kesho. Maisha yanaenda kasi sana na yamekwenda kasi kweli kwa kinda wa Manchester United, Marcus Rashford ambaye imebainika kuwa alikuwa si lolote wala chochote kabla ya kuanza msimu huu.
Kinda huyo mzaliwa wa Kusini mwa Jiji la Manchester imebainika kuwa hakuweza kufuzu katika kundi la wachezaji wa Manchester United ambao walistahili kupewa magari ya bure ya Kampuni ya Chevrolet
Kinda huyo mzaliwa wa Kusini mwa Jiji la Manchester imebainika kuwa hakuweza kufuzu katika kundi la wachezaji wa Manchester United ambao walistahili kupewa magari ya bure ya Kampuni ya Chevrolet inayoidhamini klabu hiyo.
MASKINI
wa leo ndiye tajiri wa kesho. Maisha yanaenda kasi sana na yamekwenda
kasi kweli kwa kinda wa Manchester United, Marcus Rashford ambaye
imebainika kuwa alikuwa si lolote wala chochote kabla ya kuanza msimu
huu.
Kinda huyo mzaliwa wa Kusini mwa Jiji la Manchester imebainika kuwa hakuweza kufuzu katika kundi la wachezaji wa Manchester United ambao walistahili kupewa magari ya bure ya Kampuni ya Chevrolet inayoidhamini klabu hiyo.
Rashford ameuteka ulimwengu wa soka baada ya kufunga mabao manne muhimu ya Manchester United ndani ya mechi mbili tu muhimu dhidi ya Midtjylland ya Denmark katika michuano ya Europa kisha dhidi ya Arsenal Jumapili jioni.
Hata hivyo, mpaka sasa kinda huyo anaendesha gari la bei rahisi aina ya Audi ambapo analipia kodi, bima na gharama za kupaki licha ya kuwa na mshahara mdogo wa Pauni 500 kwa wiki kama mchezaji wa timu ya vijana ya Man United.
Hata hivyo, Marcus ambaye bado anaishi na wazazi wake anatarajiwa kupewa mkataba mpya na Manchester United ambao utafikia kiasi cha Pauni 15,000 hadi 20,000 kwa wiki baada ya kuonyesha mambo makubwa ndani ya siku chache huku Man United ikihofia pia kumpoteza kinda huyo kwa timu nyingine kubwa.
“Wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wanapewa magari bure na Kampuni ya Chevrolet lakini Marcus ndio kwanza amejitokeza sasa na hakupewa gari na kampuni hiyo. Hata hivyo, jambo hilo litabadilika haraka na watu wa masoko wa Kampuni ya Chevrolet watamtafuta kumpa gari analotaka,” alisema mtu mmoja wa ndani Manchester United.
Licha ya kupewa bure magari ya kifahari aina ya Chevrolet, wachezaji wengi mastaa wa Man United kama Wayne Rooney wamekuwa hawayatumii magari hayo mara kwa mara na badala yake wamekuwa wakiendesha magari yao ya kifahari ya binafsi kama Range Rovers na Porsches.
Juzi picha zilisambaa zikimuonyesha Rashford akiwasili shuleni kwake Mersey kwenda kufanya mtihani wa somo la Chemistry akiwa na gari lake la kimaskini ikiwa ni siku moja tu baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Arsenal.
Kocha wa Man United, Louis van Gaal amekiri kwamba kuibuka kwa kinda huyo imekuwa kama zali kwake na kwa mchezaji binafsi na hakutarajia baada ya Rashford kufanya mazoezi mara chache sana na kikosi cha kwanza licha ya kuwekwa katika benchi mara mbili Novemba.
“Alikuwa anafanya mazoezi na kikosi cha pili. Wakati mwingine angeweza kucheza katika mechi za wachezaji 11 dhidi ya 11 na ndipo nilipomuona. Ungeweza kumuona jinsi alivyokuwa mwepesi na alikuwa anacheza kushoto na kulia.
Nilimuweka katika eneo la ushambguliaji. Huwezi kujua kama mchezaji anaweza kuzoea ugumu wa timu yako. Alifanya vizuri,” alisema Van Gaal.
“Mara ya kwanza haiwi vigumu kwa sababu mchezaji anakuwa makini. Lakini sasa hivi kutakuwa na presha kubwa kwa sababu watu wataanza kumuangalia tofauti.
credit- mwanaspoti

Reviewed by The Choice
on
10:54:00 AM
Rating:
No comments: