January Makamba Hatihati Kutumbuliwa Jipu Kwa Ufisadi......Mange Kimambi Aapa Kupeleka Ushahidi TAKUKURU
Sakata
la Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano),
January Makamba na Mdogo wake Mwamvita kudaiwa kupokea rushwa kutoka kwa
raia wa Italia, Vincenzo Cozzolino ili wamsaidie kupata zabuni ya
ujenzi limechukua sura mpya.
Sauti na jumbe mbalimbali zilizosambazwa na kuwekwa kwenye mtandao na mtu maarufu kwenye mitandao ya kijamii na mmiliki wa tovuti ya U-Turn, Mange Kimambi, raia wa Tanzania aishie Marekani, zinaonesha mazungumzo kati ya watatu hao, mwaka 2011. Jana, Mwamvita na Makamba walikiri kuwa sauti hizo ni za kweli.
Muitaliano
huyo ambaye anadaiwa kumpa Mange Kimambe ushahidi wote wa mawasiliano
kati yake na Ndugu hao, amejitokeza na kuwasafisha akidai kuwa hakuwahi
kuwapa rushwa wala kuhusiana na January kibiashara.
Cozzolino
ameandika ujumbe akidai kuwa ingawa yeye na Mwamvita walikuwa na
uhusiano wa mapenzi mwaka 2011 na baadae kujiingiza katika biashara
binafsi ambayo ilipelekea kugombana kwao, hawakumhusisha January kwa
aina yoyote katika biashara yao.
“Sikuwahi
kumuomba [January] kunisaidia katika biashara zangu. Sikuwahi kumpa
fedha. Mara chache nilizokutana naye ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida ya
kijamii. Nilikuwa na uhusiano na Mwamvita. Uhusiano wetu ulikuwa bomba
mwanzoni lakini ukawa na mwisho mbaya,” ameandika Cozzolino.
Awali,
sauti ya January na mwandishi wa habari iliyosambazwa, January
anasikika akieleza kuwa aliwahi kukutana mara moja Dubai na Muitaliano
huyo na kwamba alitambulishwa kama mpenzi wa dada yake.
Alisema
baadae dada yake alimwambia wameanza kufanya biashara ya kahawa na
Muitaliano huyo na baadae biashara hiyo kufa huku ikiwaacha katika
mzozo.
Kwa
mujibu wa Kamamba, Muitaliano aliyekuwa ameweka nusu ya mtaji ambayo ni
dola milioni 50, alianza kudai kiasi hicho cha fedha na sio
vinginevyo.
Alisema
kuwa awali, muitaliano huyo alikuwa anajaribu kumshawishi Mwamvita
amkutanishe na viongozi wakubwa wa serikali ikiwa ni pamoja na Katibu
Mkuu.
Hata
hivyo, Mange Kimambe ambaye ndiye anayeeleza kuwa na nyaraka zote za
ushahidi aliokabidhiwa na Muitaliano huyo na kwamba hivi sasa Muitaliano
amelipwa na kukubaliana kumsafisha Mbunge huyo wa Bumbuli.
Mange
amesisitiza kuwa ana ushahidi wote wa January na dada yake kupokea
rushwa kutoka kwa mfanyabiashara huyo na yuko tayari kuwakabidhi
Takukuru.
January Makamba Hatihati Kutumbuliwa Jipu Kwa Ufisadi......Mange Kimambi Aapa Kupeleka Ushahidi TAKUKURU
Reviewed by The Choice
on
2:36:00 PM
Rating:
No comments: