HUYU NDO Bilionea Mtanzania Anaetaka Kuinunua BENKI ya BARCLAYS Tanzania!
Inabidi
ujue Tanzania inao watu wenye pesa zao na wanayo malengo au mipango
mikubwa zaidi ya kibiashara ambayo kama ikienda inavyotakiwa wanaweza
kuifanya nchi hii kutajwa zaidi kuwa na matajiri miongoni mwa nchi zenye
Mabilionea Afrika.
Kituo
cha Television cha Marekani CNN kilimuhoji Mtanzania huyu na kikaweka
kichwa cha habari ‘kutana na Bilionea mwenye umri mdogo Afrika‘ ni
Mohammed Dewji ambaye ameajiri watu karibu elfu ishirini na nane
kutokana na viwanda na biashara zake.
Mbunge
huyu wa zamani wa Singida mjini amesema ‘nimekua nikitaka kununua Benki
kwa miaka minne mitano iliyopita, sasa hivi nimeamua nataka kuanzisha
Benki yangu kabisa japokuwa hii ishu ya Benki ya Barclays Afrika kuuzwa
imekuja na nashawishika japo sijajua kama wanataka mnunuzi atakaeichukua
Afrika nzima‘
‘Nimeshawishika
kuinunua Barclays upande wa Afrika Mashariki na ninayo pesa tayari,
sijajua wanaiuzaje lakini sina mpango wa kuichukua Barclays yote kwa
Afrika, ningependa kuinunua upande wa Afrika Mashariki kwenye nchi za
Kenya, Uganda, Tanzania yaani kwenye nchi nne au tano hivi’ – Mo
Dewji
March
24 2016 Mohammed Dewji aliandikwa na CNN kwamba anataka kuingia kwenye
soko la ushindani Afrika na kushindana na Coca cola kupitia kinywaji
chake cha Mo Cola na namnukuu akisema ‘tunashindana na Red Bull kupitia
Mo Energy Drink’
HUYU NDO Bilionea Mtanzania Anaetaka Kuinunua BENKI ya BARCLAYS Tanzania!
Reviewed by The Choice
on
9:50:00 AM
Rating:
No comments: