HIVI NDIVYO WACHEZAJI WA GENK WALIVYO MPONGEZA SAMATTA KWA BAO LAKE LA KWANZA
WALSH (WA PILI KULIA) AKIWA NA SAMATTA PAMOJA NA WACHEZAJI WENGINE WA GENK WAKISHANGILIA USHINDI WAO DHIDI YA CLUB BRUGGE. |
Beki kisiki wa KRC Genk, Sandy Walsh amempongeza Mbwana Samatta kwa bao lake la kwanza akiwa na kikosi hicho.
Walsh
ametupia picha wakiwa na wachezaji wengine pamoja na Samatta katika
mtandao wa kijamii wa Facebook akimpongeza Samatta baada ya kufunga bao
la tatu katika mechi dhidi ya Club Brugge ikiwa ni dakika chache tu
baada ya kuingia. Katika mechi hiyo, Genk iliibuka na ushindi wa mabao
3-2.
Mtanzania
huyo amejiunga na Genk akitokea mabingwa wa Afrika, TP Mazembe ya DR
Congo ambayo kwa kiasi kikubwa aliisaidia kubeba ubingwa huo.
HIVI NDIVYO WACHEZAJI WA GENK WALIVYO MPONGEZA SAMATTA KWA BAO LAKE LA KWANZA
Reviewed by The Choice
on
11:32:00 PM
Rating:
No comments: