DIAMOND ABANDIKA PICHA YA ALIKIBA NA MR.BRUE OFISINI KWAKE
Diamond
amesema hataki kuulizwa tena kama ana bifu na msanii mwingine, amedai
hana tatizo na msanii yoyote na ndio maana hata ukienda ofisini kwake
utakuta ameweka picha za wasanii wote hata ambao amekuwa akihusishwa
kuwa na bifu nao.
“Ukija ofisini kwangu me nna kuna picha ya blue nimembandika, kuna picha ya Juma Nature, kuna picha ya Ali , kuna picha ya Prof, Jay, kuna picha ya Ray C, kuna picha ya Q chief, TID, AY, wasanii wote wakubwa ambao anajua walianza katika huu muziki, wana mchango katika huu muziki wote me nimewaweka” Diamond Alisema
“Ofisini kwangu tu ukiingia tu reception, ukiingia tu kunasehemu nimeweka picha za wasanii wote , siwezi kuweka wote kwasababu zisingetosha lakini kuna baadhi ya wasanii nimeweka kwasababu najua wanamchango kwenye soko la muziki wa Tanzania.” Diamond alielezea
Diamond pia amesema kuwa yeye ndio huwa anahushishwa na bifu na wasanii wengine lakini yeye hana tatizo na mtu
DIAMOND ABANDIKA PICHA YA ALIKIBA NA MR.BRUE OFISINI KWAKE
Reviewed by The Choice
on
7:34:00 AM
Rating:
No comments: