BREAKING NEWZZZ......WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI
Waziri wa zamani wa Rwanda Jacques
Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada
ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Rwanda imesema
marehemu Jacques alikuwa ameshikiliwa kinyume cha sheria na Balozi wa
nchi hiyo nchini Ubelgiji ameandika na kusema kushikiliwa kwa Jacques na
kuita ni kifo cha mauaji.Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchuliwa katika gereza kupelekwa hosptali baada ya kuugua.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.
BREAKING NEWZZZ......WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI
Reviewed by The Choice
on
7:44:00 AM
Rating:
No comments: