AY na Prezzo wasababisha mapenzi ya Dayna Nyange na mchumba wake yavunjike
Dayna anasema picha hiyo alipiga na wasanii hao kabla hajawa maarufu wala kujihusisha na muziki kwa kiasi kikubwa hivyo hiyo ilikuwa sehemu ya kutafuta marafiki wa kumsaidia kimuziki.
“Kutokana na picha hiyo mchumba wangu huyo alihisi kwamba mmoja wa wasanii hao labda natoka naye kimapenzi hivyo akawa hataki nipige picha na wasanii na nisijihusishe tena na masuala ya kimuziki.
“Muziki ni kitu ninachokipenda sana katika maisha yangu hapo nikaona wivu umezidi kwa mwezangu ambaye tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kike mwenye miaka 10, tukaamua kuachana nami nikaendelea na muziki wangu hadi leo bila mchumba, mpenzi wala nini na maisha yanaenda,” alijieleza mrembo huyo.
Dayna alianza kujulikana katika muziki mwaka 2008 baada ya kuimba wimbo wa ‘Mafungu ya Nyanya’ na msanii aliyewika katika kampeni ya urais na wabunge mwaka 2005, Marlow, kisha akatoa ‘Nivute kwako’ na sasa anatamba na wimbo wa ‘Ungejua’.
AY na Prezzo wasababisha mapenzi ya Dayna Nyange na mchumba wake yavunjike
Reviewed by The Choice
on
10:51:00 PM
Rating:
No comments: