AY aitaja sababu kubwa iliyo sababisha akaachana na aliyekuwa mpenzi wake Amani mwaka 2007

Baada ya miaka kadhaa kupita baada ya nyota wa Zigo, Rapper Ambwene Yessaya a.k.a AY kutoka Tanzania ametaja sababu iliyopelekea kwa yeye na mwanamuziki Amani wa Kenya kuachana katika penzi lililodumu kwa muda wa miaka miwili.

Miaka miwili ni mingi kwa mahusiano kudumu haswa kwa mastaa ambao wanakuwa wakitamaniwa na kila mwenye tamaa ya kutaka kuwa naye. Kuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu kiasi walicho fikia wawili hao watu wengi walishangazwa na wawili hao kwanini waliachana huku wote wakiwa sio watu wa kuwa kwenye skendo mara kwa mara.

Na kwanzia wawili hawa waachane hakuna hata mmoja wao ambaye aliamua kuweka wazi kwanini wameachana huku kukiwepo maneno ya chini kwa chini yasio kuwa na ukweli au uhalisia wa kuachana kwa wawili hao kwanzia mwaka 2017.

Lakini rapper AY amejitokeza nakuweka wazi kisa cha kuachana na Amani ambaye walianza mahusiano mwaka 2005. AY anasema walikutana na Amani mwaka huo kisha kuwa marafiki hadi wapenzi, Walipendana hadi wakati wanaachana mwaka 2007. Sio mizozo, usaliti au dalili za kuchokana ambazo zimepelekea kuwachana kwa wawili hawa.

Umbali wa wapenzi hawa ikiwa AY ni Mtanzania na Amani ni mtu wa Kenya, wawili hawa walifikia hatua ya kutaka kuishi pamoja ili kukuza mahusiano yao wakiwa karibu kutokana na mapenzi walio kuwa nayo.

Lakini ilikuwa ngumu kwa ni nani atoke kwenye nchi yake aje aishi kwenye nchi ya mwezake kisa penzi. Amani ni mmoja wa wasanii ambaye huwezi kuema lolote baya juu ya nchi ya Kenya na akakuangalia bila kukuchana live zako, Huku AY naye ni mmoja wa wasanii ambaye anapambana kutangaza jina la Tanzania ili ipate heshima nje ya nchi.

Hakuna hata mmoja ambaye alikuwa tayari kwenda kwenye nchi ya mwingine ili achukue uraiya na kukuza penzi nakuacha heshima ya utaifa wake. Sababu hiyo ndiyo imekuwa chahcu cha kuachana kwa AY na Amani
AY aitaja sababu kubwa iliyo sababisha akaachana na aliyekuwa mpenzi wake Amani mwaka 2007 AY aitaja sababu kubwa iliyo sababisha akaachana na aliyekuwa mpenzi wake Amani mwaka 2007 Reviewed by The Choice on 2:18:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.