Akamatwa na polisi akiwa na kichwa cha mtoto karibu na kitua cha mabasi
Polisi huko Moscow wamemkamata mwanamke baada ya kupatikana amebeba kichwa cha mtoto.
Kanda ya video inamuonesha mwanamke huyo akitembea karibu na kituo cha basi akiwa amebeba kichwa hicho mikononi. Alikamatwa na polisi na kupelekwa kufanyiwa uchunguzi wa akili.
Mwanamke huyo Gyulchekhra Bobokulova, kutoka jamhuri ya Uzbekistan anatuhumiwa kwa kumuua mtoto huyo msichana kabla ya kuchoma moto nyumba ya wazazi wake. Picha za CCTV zinaonesha mwanamke huyo aliyevalia hijab akitembea nje ya kituo cha usafiri akiwa amebeba kichwa cha mtoto.
Afisa mmoja wa ulinzi anaonekana akimkabili na kumbwaga sakafuni kabla ya kumfunga pingu. Bi Bobokulova amekamatwa na sasa anafanyiwa uchunguzi wa kiakili kubaini iwapo ana uwezo wa kubaini vitendo vyake.
Taarifa kutoka kwa afisi ya upelelezi wa jinai mjini Moscow inasema ’’ maafisa wameanzisha shughuli ya kubaini chanzo cha kifo cha mtoto ambaye kiwiliwili chake kilipatikana katika kitongoji cha Narodnoye Opolcheniye Magharibi mwa Moscow’’.
Kwa mujibu wa jarida la kirusi la Life News, mwanamke huyo aliulizwa na
askari polisi wa kituo cha usafiri cha Oktyabrskoye Polye, kitambulisho
chake. Hapo ndipo alipogutuka na kutoa kichwa cha mtoto huyo kutoka
kwenye mkoba wake na kusema kwa sauti ya juu kuwa yeye ni gaidi na kuwa
alikuwa malaika wa kifo na kuwa angejilipua
Kanda ya video inamuonesha mwanamke huyo akitembea karibu na kituo cha basi akiwa amebeba kichwa hicho mikononi. Alikamatwa na polisi na kupelekwa kufanyiwa uchunguzi wa akili.
Mwanamke huyo Gyulchekhra Bobokulova, kutoka jamhuri ya Uzbekistan anatuhumiwa kwa kumuua mtoto huyo msichana kabla ya kuchoma moto nyumba ya wazazi wake. Picha za CCTV zinaonesha mwanamke huyo aliyevalia hijab akitembea nje ya kituo cha usafiri akiwa amebeba kichwa cha mtoto.
Afisa mmoja wa ulinzi anaonekana akimkabili na kumbwaga sakafuni kabla ya kumfunga pingu. Bi Bobokulova amekamatwa na sasa anafanyiwa uchunguzi wa kiakili kubaini iwapo ana uwezo wa kubaini vitendo vyake.
Taarifa kutoka kwa afisi ya upelelezi wa jinai mjini Moscow inasema ’’ maafisa wameanzisha shughuli ya kubaini chanzo cha kifo cha mtoto ambaye kiwiliwili chake kilipatikana katika kitongoji cha Narodnoye Opolcheniye Magharibi mwa Moscow’’.
"'Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa yaya aliyekabidhiwa jukumu la
kumtunza mtoto huyo mwenye umri kati ya miaka 3-4 alisubiri hadi wazazi
wake na kakake mkubwa wakaondoka kabla ya kumuua na kisha kuchoma moto
nyumba yao’’.
''Chanzo cha tukio hilo kwa hakika hakijabainika ila tumemkamata yaya
huyo ambaye alizaliwa mwaka wa 1977 katika jamhuri ya Uzbekistan,''
taarifa hiyo iliongezea. Afisa mwengine wa polisi ambaye hakutaka
kutajwa anasema kuwa ''mtoto huyo alichinjwa na kiwiliwili chake
kikachomwa moto. Kichwa chake hakikupatikana kwenye eneo la tukio.''
Akamatwa na polisi akiwa na kichwa cha mtoto karibu na kitua cha mabasi
Reviewed by The Choice
on
6:33:00 AM
Rating:
No comments: