Wajenga choo cha milioni 8.7 ili mtoto wa mfalme akitumie katika ziara yake na hakikutumika
Choo kilichogharimu takriban dola 4000 sawa na shilingi ya KItanzania
8750,8000 (Milioni 8.75) kilichojengwa kwa ajili ya mtoto wa mfalme wa
Thailand aliyefanya ziara nchini Cambodia, hakikutumika kabisa, wamesema
maafisa. Imeripotiwa kuwa mwanamfalme Maha Chakri Sirindhorn alipiga
picha tu choo hicho wakati akiwa ziarani Yeak Lom Lake, kaskazini
mashariki mwa Cambodia.
Choo hicho sasa kimeondolewa, na chumba chenyewe kitafanywa kuwa ofisi ya utalii. Habari hii iligonga vichwa vya habari nchini Cambodia, ambapo chini ya asilimia 40 ya watu wanaoishi vijijini wana vyoo. Choo hicho, ambacho kilikuwa na kiyoyozi, kilijengwa kwa ajili ya ziara ya saa mbili ya Bi Sirindhorn katika eneo hilo. "Hakuingia chooni, alitazama akiwa nje na kupiga picha kadhaa," amesema mkuu wa jamii Ven Churk, akizungumza na shirika la habari la AFP. Gharama za ujenzi zililipiwa na Thailand, wamesema maafisa wa Cambodia.
Choo hicho sasa kimeondolewa, na chumba chenyewe kitafanywa kuwa ofisi ya utalii. Habari hii iligonga vichwa vya habari nchini Cambodia, ambapo chini ya asilimia 40 ya watu wanaoishi vijijini wana vyoo. Choo hicho, ambacho kilikuwa na kiyoyozi, kilijengwa kwa ajili ya ziara ya saa mbili ya Bi Sirindhorn katika eneo hilo. "Hakuingia chooni, alitazama akiwa nje na kupiga picha kadhaa," amesema mkuu wa jamii Ven Churk, akizungumza na shirika la habari la AFP. Gharama za ujenzi zililipiwa na Thailand, wamesema maafisa wa Cambodia.
Wajenga choo cha milioni 8.7 ili mtoto wa mfalme akitumie katika ziara yake na hakikutumika
Reviewed by The Choice
on
10:40:00 AM
Rating:
No comments: