HAYA NDIYO YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE
Baada
ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha
kuwataka waandishi wote wa habari za kiuchunguzi pamoja na watafiti
kuweka hadharani na kuueleza umma kile kilichotokea Zanzibar, Waandishi
na watafiti mabalimbalai wamejitokeza na vielelezo vinavyoeleza jinsi
uchaguzi huo ulivyoharibika
Vielelezo
hivyo ni Nakala za fomu namba MUR. 12A za matokeo zilizotoka katika
vituo vya kujumuisha kura ambazo zilikuwa zimejazwa kimakosa.
Hii
ni fomu kutoka Kituo cha Skuli ya Mabaoni namba 23801, Jimbo la Chonga
namba 2909 fomu hii siyo halali kutokana na kukosa mhuri wa tume ya
uchaguzi Zanzibar. Msimamizi wa kituo ni Khamis mkungwa Zaid.
Fomu nyingine inatoka katika kituo cha Urusi chenye namba 26503, katika jimbo la Jang’ombe namba 1940
A. Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008
Hii
ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008, Jimbo la Mkwajuni namba
1926, fomu hii imepoteza uhalali kwasababu imefutwafutwa na haina mhuri
wala jina la msimamizi wa kituo.
B. Kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi
Hii
ni fomu kutoka katika kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi namba 21618,
Katika jimbo la Chumbuni namba 1931, fomu hii imekosa uhalali kwasababu
imefutwa majina ya mawakala na kupandikizwa majina mengine juu ya
maandishi ya kivuli.
C. Jimbo la Chumbuni namba 1937
Hizi
mbili, fomu kutoka kiwanja cha mpira Masumbani namba 29304 kutoka
jimbo la Chumbuni namba 1937, fomu hii inakosa uhalali kwa sababu haina
mhuri , maandishi ya meandikwa tena kwa kalamu juu ya maandishi ya
kivuli na saini imewekwa zaidi uya mara moja. Fomu ya pili ni kutoka
jimbo la Chakechake jina la kituo na namba haisomeki, fomu hii inakosa
uhalali kwasababu inamhuri ambao siyo wa Tume ya uchaguzi anzibar ni
mhuri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ambao haupaswa kutumika katika
fomu hii.
D. Mihuri ya kughushi
Fomu
ya pili ni kutoka jimbo la Chakechake jina la kituo na namba haisomeki,
fomu hii inakosa uhalali kwasababu ina mhuri ambao siyo wa Tume ya
uchaguzi anzibar ni mhuri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ambao
haupaswa kutumika katika fomu hii.
Matumizi ya Mihuri Bandia katika karatasi za kujumuishia matokeo ya wagombea nafasi ya Rasi wa Zanzibar.
E. Fomu zimejirudia zaidi ya mara moja
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa ZEC alisema utata wa matokeo ulianza pale
wajumbe waliopelekwa Pemba kurudi na kuiarifu Tume dhidi ya matendo
yaliyofanywa na wasimamizi wa ZEC Pemba hata hivyo wakati uchunguzi na
mabishano yakiendelea Mmoja wa wagombea akaitisha wanahabari na
kujitangaza ameshinda kwa matokeo ambayo kila mmoja wetu alishangaa
sana,
Ni
kitendo cha aibu na Fedheha kubwa wanaoshabikia hawakuona madhara
yake,sijui alitoa wapi Takwimu ambazo zilitoa ushindi kwa wagombea
wawili tu,tena ukijumlisha asilimia ni 100 inasikitisha sana,Shinikizo
la kunitaka nimtangaze mshindi kinyume na taratibu lilinifanya niubebe
msalaba kusimamisha na kufuta matokeo baada tu ya kuitisha fomu chache
za uthibitisho mwandishi haya ndio tuliyakuta,Ni nusu ya uchaguzi wote
kila jimbo ulichezewa
Tumejiridhisha
watu wetu watendaji wa ZEC walio apa walifanya haya,kutumia mihuri ya
Bandia kujaza hizi fomu kinyume na taratibu kama mnavyo ona alisisitiza
Mzee Jecha kwa masikitiko akiwaonyesha waanndishi waliofika kuhoji nini
kilitokea hasa.
HAYA NDIYO YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE
Reviewed by The Choice
on
9:12:00 PM
Rating:
No comments: