MH PAUL MAKONDA AFANIKISHA MPANGO WA KUWASAFIRISHA WALIMU BURE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na waandishi wa
habari kwenye hoteli ya Lamada Posta jijini Dar es salaam leo wakati
alipozungumzia mpango wa kuwasafirishwa walimu bure jijini Dar es salaam
wakati wa kwenda na kurudi kazini huku akiwa ameongozana na viongozi wa
vyama vya usafirishaji wa abiria jijini Dar es salaam pamoja na
viongozi wa Madereva wa Daladala jijini Dar es salaam, kutoka kulia
ni Makamu mwenyekiti waUmoja wa Madereva, Shabani Mdemu na katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam, (Uwadar), William Masanja
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda wa pili kutoka kushoto
akimsikiliza Said Mabrouk Mwenyekiti wa Chama Chama Wamiliki wa
Daladala Mkoa wa Dar es salaam wakati akizungumzia mwitikio wa wamiliki
hao kuhusu kuwasafirisha walimu ili kuunga mkono juhudi za Mkuu wa
Wilaya ya Konondoni Mh. Paul makonda na Rais Dk. John Pombe Magufuli
katika kutoa elimu bure hapa nchini.
Moja
ya jambo ambalo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi makini wa
Mheshimiwa John Pombe Magufuri imelifanya kuwa kipaumbele kikubwa kwenye
mipango yake ya kimaendeleo ni suala la uboreshaji wa sekta ya elimu
nchini na ndio maana serikali imeanza utekelezaji wa mpango huu kwa
kufuta ada zote mashuleni.
Kimsingi
ni ndoto hii ya Mheshimiwa Raisi ambayo nina hakika kila mmoja wetu
anaelewa ukubwa wa faida zake kwenye ujenzi wa Tanzania mpya na yenye
wasomi na wataalamu wa kila namna tena wanaopatikana bila kuzingatia
hali ya kipato cha familia anayotokea mwanafunzi, iliyonifanya mimi kama
msaidizi wake katika nafasi ya ukuu wa wilaya nijiulize kila wakati juu
ya ushiriki wangu wa kuhakikisha inatimia kikamilifu. Maswali ambayo
yamenifikisha kwenye wazo la kuboresha sekta hii kwa kuchagua kufanya
jambo ambalo wakati serikali ikiendelea kupigania changamoto nyinginezo
za kuboresha ajira za walimu ikiwemo upandishwaji wa madaraja na
mishahara, basi na mimi katika nafasi yangu nishiriki kwenye mchakato
huu mzima kwa kutoa motisha ya usafiri wa bure kwa walimu wote
wanaofundisha kwenye shule za serikali zilizopo jijini Dar es Salaam.
Kwa
ufupi ni kwamba, wazo hili limejengwa juu ya msingi wa sababu kubwa
tatu. Moja, kwa kuzingatia changamoto za nauli za mara kwa mara
wanazolazimika kuzilipa walimu ili kuyafikia kwa wakati maeneo yao ya
kufanyia kazi na pili, ni kuhakikisha mimi na serikali yangu ya wilaya
ya Kinondoni tunakuwa sehemu ya juhudi za Mheshimiwa Raisi za kuboresha
maslahi na mazingira ya walimu ya kufanyia kazi ili matarajio ya ndoto
yake anayoipigania usiku na mchana ya kutaka kuiona sekta ya elimu
nchini ikikua kwa kasi yanatimia. Na tatu, ni kuwafanya walimu wa wilaya
ya Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla kama watumishi wenzangu wa
serikali nao wanafaidi sehemu ya matunda ya serikali yao ambayo kwa
dhati imedhamiria kubadilisha maisha yao ili na wao waweze kubadilisha
maisha ya vijana wetu kupitia taaluma.
Kwasababu
hizo nilizozianisha hapo juu ninaomba kuwatangazia walimu wangu wa
shule zote za serikali kuanzia za msingi mpaka sekondari ya kwamba, sasa
watasafiri bure wanapokwenda kutufundishia wadogo zetu na watoto wao.
Hii ni baada ya kufanya vikao na mazungumzo ya kina na wamiliki wa
vyombo vya usafiri wa umma kupitia vyama vyao vya Darcoboa na Uwadar na
hatimaye mazungumzo hayo kuitimishwa na mkutano wa vyama vyote hivyo
viwili vya wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao kwa sauti moja
wamekubali kuniunga mkono kwenye utekelezaji wa wazo langu hili.
Kipekee
na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru sana
wamiliki hawa wa vyombo vya usafiri wa umma pamoja na viongozi wa vyama
vya Darcoboa na Uwadar kwani walikuwa na kila sababu ya kukataa hasa
ukizingatia kuwa wao ni wafanyabiashara na tena wanazo changamoto nyingi
katika sekta yao ya usafirishaji, wengine wakiwa hata wamekopa kwenye
mabenki ili wapate uwezo wa kufanya biashara, lakini kwenye jambo hili
wote kwa umoja wao wameseme ndio na wako tayari kuanza haraka
iwezekanavyo.
Utaratibu
kwa walimu juu ya utumiaji wa fursa ambayo tumeipata utakuwa kama
ifuatavyo:- Moja, nimemuelekeza ofisa elimu wa sekondari na shule za
msingi, kutoa maelekezo kwa wakuu wa shule zote za serikali zilizopo
wilayani kwangu na wilaya nyinginezo za jiji la Dar es Salaam,
kutengeneza vitambulisho vya shule zao vitakavyokuwa na picha ya
mwalimu, jina lake kamili, jina la shule anayofundisha, namba ya simu ya
mkuu wa shule husika pamoja na saini yangu mimi mwenyewe Paul Makonda
ili kuepuka udanganyifu.
Nimewataka
zoezi hili walifanye na kulikamilisha ndani ya wiki moja ambapo baada
tu ya kukamilika itakuwa ni furaha yangu kuwatangazia walimu wote wa
shule za serikali jijini Dar es Salaam kuwa, watakuwa wakipanda daladala
bure ila tu kwa siku za jumatatu mpaka Ijumaa na kwa muda wa saa kumi
na moja asubuhi mpaka saa mbili asubuhi na kati ya saa tisa mpaka saa
kumi na mbili jioni. Ingawa, kila mwalimu atalazimika kuonyesha
kitambulisho chake alichotengenezewa kwenye shule yake pamoja na kile
cha ajira ya serikali.
Imetolewa na:-
Paul Makonda
Mkuu wa wilaya – Kinondoni.
MH PAUL MAKONDA AFANIKISHA MPANGO WA KUWASAFIRISHA WALIMU BURE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM
Reviewed by The Choice
on
10:16:00 AM
Rating:
No comments: