JE WAJUA WATOTO WA WILL SMITH HULALA NA NYOKA 10, WENGINE HAWAJAFUNGWA
Watoto wa Will na Jada Smith, Willow na Jaden wana mengi ya ndani ambayo wengi walikuwa hawayafahamu.
Kwa
mujibu wa US Weekly, Willow Smith mwenye umri wa miaka 13 hulala na
nyoka kumi chumbani kwake na baadhi yao hawajafungwa kabisa!
Lakini
sio pekee ambaye ana mapenzi na nyoka hao, kaka yake Jaden pia
huwachukulia nyoka wa dada yake kama wapenzi wake kwa kuwa huwa
wanaingia chumbani kwake na kulala nae kitandani huku wakijizungusha
mwilini kwake!
Willow ameshawazoea nyoka hao kwa kuwa alianza kuishi na nyoka wa kwanza mwaka 2008 wakati akiwa na umri wa miaka 7 tu.
Jada
Pinkett aliwahi kulimbia jarida la Rebok mwaka jana kuwa yeye
anawapenda sana nyoka na mwanae Willow pia amekuwa anawapenda daima.
“Anaweza
kwenda kwenye store ya nyoka akachukua nyoka mmoja na akajizungushia.
Sikuwahi kumgusa nyoka hapo kabla, na nilikuwa siwezi
kuwashika…..nimekuwa nampenda Willow daima tangu mwanzo. Nilimwambia
Willow, ‘umemfanyia mama msaada mkubwa. Umenisaidia kushinda uoga’..”
JE WAJUA WATOTO WA WILL SMITH HULALA NA NYOKA 10, WENGINE HAWAJAFUNGWA
Reviewed by The Choice
on
10:55:00 PM
Rating:
No comments: