ETIHAD YAPATA TUZO YA HESHIMA YA KIFEDHA
Shirika la ndege la Etihad limepokea tuzo ya heshima katika mabadiliko ya kifedha kwa mwaka 2015 kutoka kwa kampuni ya kimarekani ya Innovation Enterprise inayoongoza kwenye masuala ya uvumbuzi katika sekta uwekezaji.
Tuzo hiyo ilitolewa kwa Shirika la Ndege la Etihad ambalo lilifanikiwa kuzishinda kampuni nyingine kupitia kituo chake cha nje cha mpango wa Mabadiliko ya kifedha. Programu hiyo iliundwa mahususi kwa ajili ya shughuli za utendaji na uendeshaji wa shirika hilo katika mazingira ya gharama nafuu.
James Rigney, Afisa Mkuu wa fedha wa shirika la ndege la Etihad alisema…”Tunajisikia fahari kupokea tuzo hii kwa kazi kubwa iliyofanywa na Timu yetu ya mipango ya fedha. Tulikuwa na muda mfupi tu wa miezi sita katika kuhakikisha tunatekeleza mabadiliko ya mpango wetu, na juhudi yao kwenye kazi hii ulitufanya tuweze kupunguza nguvu kazi kifedha, kuanza kusonga mbele na muundo wa kikanda uliopunguza gharama na kukuza kipato hadi kufikisha dola za kimarekani milioni 28 kama akiba huku lengo likiwa kufikia dola za kimarekani milioni 50 milioni hadi mwisho wa mwaka huu.”
Awamu ya kwanza ya kituo cha nje cha mpango wa Mabadiliko ya kifedha kilihitaji kuundwa kwa kituo kimoja chenye ubora kitakachoshughulikia miamala yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1 kutoka nchi zaidi ya hamsini. Awamu ya pili ilitazamia shirika la ndege la Etihad kupitisha mipango ya kuboresha michakato muhimu na kuondoa vikwazo, ili kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika kituoni hapo bila kukiuka viwango vya juu vya kuongoza ndege
Shirika la Innovation Enterprise ndio linaongoza katika kukuza ubunifu katika mipango ya fedha na taaluma ya uchambuzi, na ni mratibu mkubwa wa matukio katika sekta ya Mipango ya fedha na uchambuzi.
***MWISHO***
Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com
ETIHAD YAPATA TUZO YA HESHIMA YA KIFEDHA
Reviewed by The Choice
on
10:47:00 AM
Rating:
No comments: