BREAKING NEEWS; MWANAMUZIKI MKONGWE KASSIM KIPILI AFARIKI DUNIA
Mwanamuziki mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili akicharaza nyuzi za Gitaa lake chini ya Kundi zima la Mjomba Band.
MWANAMUZIKI
mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili amefariki dunia akiwa chumbani
kwake, Tabata jijini Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Chama cha Muziki wa
Dansi (CHAMUDATA) Hassan Msumari, amesema kuwa kifo cha Mapili
kimegunduliwa usiku huu baada ya mlango wa chumba chake kuvunjwa.
Mlango huo ulivunjwa baada ya Kassim Mapili kutoonekana tangu alipokwenda kutazama mpira wa Arsenal na Barcelona Jumanne usiku.
Kwa
mujibu wa Msumari, mara mlango ulipovunjwa Kassim Mapili alionekana
akiwa ameshafariki akiwa amejifunga taulo, ishara inayoonyesha kuwa
aidha alikuwa anakwenda kukoga au ametoka kukoga.
Jumatatu
jioni Kassim Mapili alishiriki vizuri mazishi ya mwanahabari Fred Mosha
makaburi ya Kinondoni ambapo alipewa wasaa wa kuongea machache na kama
vile hiyo haitoshi, Mapili aliimba makaburini hapo kuomboleza kifo cha
Fred Mosha
BREAKING NEEWS; MWANAMUZIKI MKONGWE KASSIM KIPILI AFARIKI DUNIA
Reviewed by The Choice
on
11:17:00 PM
Rating:
No comments: