Ben Pol aitaja hii sababu kuwa ndio maana hatofuga rasta, kuvaa hereni au kujichora tattoo

Benard Paul ‘Ben Pol’ amesema  hapendi na hatauchora ‘tattoo’ mwili wake kama baadhi ya wasanii na watu maarufu wafanyavyo kwa kuwa anauheshimu sana.

Ben Paul alisema imekuwa ni kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii kujichora ‘tattoo’ na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake jambo hilo halina nafasi.

“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano wa tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwa sababu nauheshimu mwili wangu, ndiyo maana nipo kawaida kila wakati,” alifafanua.

Msanii huyo aliongozana na msanii mwenzake, Juma Musa ‘Jux’ walipotembelea ofisi za Kampuni ya New Habari (2006) Ltd kwa lengo la kutangaza wimbo wao mpya wa ‘Nakuchana’
Ben Pol aitaja hii sababu kuwa ndio maana hatofuga rasta, kuvaa hereni au kujichora tattoo Ben Pol aitaja hii sababu kuwa ndio maana hatofuga rasta, kuvaa hereni au kujichora tattoo Reviewed by The Choice on 11:48:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.