Ali Kiba kwenda Nigeria mwezi ujao, huyu ndiye msanii atakayefanya nae kolabo.
Msanii huyo anayetamba na kibao cha ‘Right Now’, aliwaambia waandishi wa habari jambo hilo wakati alipokuwa akizungumzia ziara yake ya kikazi nchini Tanzania.
“Kwa Tanzania namkubali sana Ali Kiba na Christian Bella,” alisema Seyi Shay. “Nimezungumza na Ali Kiba na kukubaliana tufanye kazi pamoja, anatarajiwa kuja Nigeria, Machi mwaka huu kwa ajili ya kukamilisha mchakato huo.”
Seyi Shay ni balozi wa Pepsi nchini Nigeria na alikuja Tanzania kwa mwaliko rasmi wa kampuni hiyo nchini na alifanya shoo moja mkoani Mwanza kabla ya kutembelea kiwanda cha Pepsi jijini Dar es Salaam kisha kurudi nchini kwao
Ali Kiba kwenda Nigeria mwezi ujao, huyu ndiye msanii atakayefanya nae kolabo.
Reviewed by The Choice
on
10:06:00 AM
Rating:
No comments: