TASWIRA MSIBA WA NDANDA KOSOVO
Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) samabamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda wakiwa msibani hapo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Ndanda Kosovo, King Dodoo akiweka mambo sawa msibani.
King Blaise wa FM Academia akiimba kwa huzuni.
Mama yake Ndanda Anne Mariane Kombe akilia kwa uchungu. Mke wa pili wa marehenu, Infrancie.
Francie akilia mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mumewe.
Mmoja wa waombolezaji akilia kwa uchungu.
Totoo Zebingwa akimsalimia
WAZIRI
wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye pamoja na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda wamewaongoza mamia ya
waombolezaji katika shughuli ya mazishi ya staa wa Muziki aliyefariki
mwishoni mwa wiki iliyopita, Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ katika Makaburi ya
Kinondoni jijini Dar,
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya mwanamuziki huyo, King
Dodoo marehemu anatarajiwa kuzikwa leo Jumatano kwenye Makaburi ya
Kinondoni jijini Dar ambapo maandalizi yamefanyika kwenye nyumba ya
Ubalozi wa Congo DRC iliyopo Kinondoni-Hananasif jijini.
Dodoo
alisema wameamua kumzika marehemu hapa nchini kufuatia wosia wake
alioutoa mbele ya Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo,
Nape Nnauye wakati akizungumza na wanamuziki wa dansi katika Ukumbi wa
Vijana Kinondoni mwezi uliopita.
Katika
kikao hicho Ndanda alisimama na kusema endapo akifa basi maiti yake
izikwe hapa Tanzania kwa kuwa ndipo mahali alipopatia mafanikio makubwa
ya kimuziki na anahisi ndiyo sehemu ambayo atazikwa na watu wengi kuliko
Lubumbashi alikozaliwa
TASWIRA MSIBA WA NDANDA KOSOVO
Reviewed by The Choice
on
4:19:00 PM
Rating:
No comments: