Pam D alia na Chid Benz
Pamela Daffa ‘Pam D
Na Mayasa Mariwata
MKALI wa Bongo
Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ amesema kuwa, hali aliyonayo Rashid Makwiro
‘Chid Benz’ kwa sasa kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya imekuwa
ikimnyima usingizi kwa kuwa ni moja ya wasanii aliokuwa anawakubali.
Akibonga
machache na Showbiz, Pam D anayebamba na Ngoma Ya Popolipopo alisema,
wasanii wengi wanaingia kwenye mkumbo huo kutokana na kutotaka kupitwa
na starehe za ujana pamoja na kuiga mambo ya wasanii wa nje matokeo yake
wanaambulia maumivu, kama ilivyo kwa Chid na wengineo.
Rashid Makwiro ‘Chid Benz’
“Huwezi amini
kuna muda huwa nakaa nikiangalia picha za Chid za kipindi cha nyuma na
huyu wa sasa najikuta machozi yakinitoka kuona kipaji kama kile
kinapotea bila sababu za msingi, kikubwa namuombea kwa Mungu aweze
kuachana na hayo mambo kabisa japo najua kuna ugumu,” alisema Pam D.
Kwa sasa Chid
yupo katika Kituo cha Life & Hope Rehabilitation Organization (Soba
House) kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani akipatiwa huduma ya kuachana na
utumiaji wa dawa za kulevya ambapo hali yake inaendelea vizuri
Pam D alia na Chid Benz
Reviewed by The Choice
on
8:45:00 AM
Rating:
No comments: