MTANGAZAJI SALIM KIKEKE APATA MTOTO WA KIUME
Salim
KIKeke si jina geni hasa ukanda wa Afrika Mashariki. Ni Mtanzania
anayetangaza vipindi mbalimbali katika shirika la Habari la Uingereza
(BBC) na mshindi wa mara mbili kwenye Tuzo za Watu kama mtangazaji wa
runinga anayependwa.
Kupitia
ukurasa wake wa Facebook , alim amewajulisha mashabiki wake kuwa yupo
katika likizo ya kulea (paternity leave) hii ni kutokana na kupata mtoto
wa kiume anayeitwa Ioan (Yoan) Issa Kikeke. Aliulizwa maana ya jina
hilo la mtoto wake wa kiume na kudai ni: Zawadi kutoka kwa Mungu.”
Huyu anakuwa ni mtoto wake wa pili.
Na hivi ndivyo alivyoandika kwenye Facebook:
Asanteni
sana kwa salaam zenu. Bado niko kwenye likizo ya uzazi. Naomba radhi
kwa wasanii wachanga kwa kushindwa kurusha kazi zenu kwa muda sasa
kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu, hali kadhalika kwa
mashabiki wa habari mbalimbali za ulimwengu pamoja na za michezo
kumekuwa kimya kidogo lakini msiwe na shaka tutaendelea hivi karibuni.
Nichukue nafasi hii pia kuwatambulisha kwa bwana mdogo Ioan (Yoan) Issa
Kikeke. Kwa mapenzi yake Mola nitarejea kazini mwisho wa mwezi huu wa
Aprili. Shukran sana na Mwenyezi Mungu awabariki sana
CHANZO na Bongo5
MTANGAZAJI SALIM KIKEKE APATA MTOTO WA KIUME
Reviewed by The Choice
on
7:50:00 AM
Rating:
No comments: