Mchina Anyongwa Ndani ya Gari Dar es Salaam..
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo wanaoishi maeneo aliyokutwa Mchina huyo zinaeleza kuwa, gari la marehemu huyo walianza kuliona hapo tangu alfajiri ya siku hiyo lakini kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo walivyozidi kulitilia shaka maana hakukuwa na mtu aliyetoka ama kuingia.
Waliendelea kusema kwamba ilipofika saa 10.00 jioni walilazimika kulisogelea na kuchungulia ndani ndipo walipomuona mtu akiwa amelala kiti cha nyuma, walipomwamsha hakuamka wala kujigeuza ndipo waliwaarifu polisi wa Kituo cha Mabatini Kijitonyama.085A9757
Moja ya msumali uliokuwa umetegwa kwenye gari hilo.
Mashuhuda hao walidai kuwa huenda Mchini huyo aliuawa kisha kutelekezwa na gari lake maeneo hayo kwani alikuwa na michubuko mikononi na shingoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Alphonce Fuime alipohojiwa na gazeti hili wiki iliyopita ofisini kwake alikiri kutokea kwa mauaji hayo.
“Huyu marehemu inaonekana alikuwa akitoka casino na uchunguzi wa awali unaonesha aliuawa sehemu nyingine na akutupwa hapo.Tunaendelea na uchunguzi kuwasaka watu aliokuwa nao casino kwa mara ya mwisho,” alisema Kamanda Fuime aliyefafanua kuwa mwili huo ulipelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mchina Anyongwa Ndani ya Gari Dar es Salaam..
Reviewed by The Choice
on
8:42:00 AM
Rating:
No comments: