Makonda awageukia Bodaboda, awaahidi pikipiki kwa Sh 3,500 kwa siku, kuingia posta

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama Bodaboda mkoani humo na kuwapa ahadi nono za kuwainua kimaisha kupitia biashara hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Makonda ameahidi kuwapa pikipiki bodaboda hao kwa marejesho ya shilingi 25,000 kwa wiki (sawa na shilingi 3,500) kwa siku na baadae kuwaachia wazimiliki wao.
Mwendesha bodaboda akiwa amepakia abiria watatu kwenye chombo hicho cha usafiri, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao, kama walivyokutwa eneo la Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam juzi.  Picha na  Joseph Zablon
Mwendesha bodaboda akiwa amepakia abiria watatu kwenye chombo hicho cha usafiri, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao, kama walivyokutwa eneo la Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam juzi. Picha na Joseph Zablon (Maktaba)
Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuwatengenezea mpango mzuri wa utakaowawezesha bodaboda hao kuingia katikati ya Jiji, tofauti na ilivyo sasa.
Ahadi ya Makonda kuwaruhusu Bodaboda kuingia Jijini ni ukamilifu wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.
Juzi, Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema) pia aliahidi kuhakikisha Bodaboda wanaweza kuingia mjini kwa utaratibu maalum.
Makonda awageukia Bodaboda, awaahidi pikipiki kwa Sh 3,500 kwa siku, kuingia posta Makonda awageukia Bodaboda, awaahidi pikipiki kwa Sh 3,500 kwa siku, kuingia posta Reviewed by The Choice on 1:47:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.