HUU NDIO MSHAHARA ANAOLIPWA MBWANA SAMATTA KATIKA CLUB YAKE MPYA YA KRC GENK
Kufanya kazi Ulaya ni raha sana kwa maana ya kupiga hatua, lakini nako kuna ugumu wake kimaslahi kama utalifikiria suala la kodi. Najua unatamani kujua maisha ya wanasoka wa Ubelgiji hususani katika kipindi hiki anachocheza soka mtanzania Mbwana Samatta nchini humo, Kwa mujibu wa mtandao wa www.xpats.com hadi kufikia April 10 2015 mishahara ya wachezaji wengi wa Ligi Kuu Ubelgiji ilikuwa inatajwa kuwa ya wastani wa euro 253,586 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya milioni 600 za kitanzania kabla ya kukatwa kodi pamoja na bima. Mshambuliaji mpya wa KRC Genk, Mbwana Samatta atakuwa akilipwa mshahara wa euro 35,600 (zaidi ya Sh milioni 85) kwa mwezi. Lakini makato ya kodi, kupitia kwa Mamlaka ya Kodi ya Ubelgiji, yanamfanya Samatta kuondoka na kiasi kidogo tu cha kodi. Taarifa za uhakika kutoka Ubelgiji zinasema, Samatta atakuwa akikatwa asilimia 48 kama utajumlisha ‘TRA ya huko’ na makato ya mshahara ya serikali ya mshahara wake. makato ambayo wanakumbana nayo wageni wengi wanaofanya kazi nchini humo. Pamoja na kulipwa zaidi ya Sh milioni 85, maana yake Samatta atakuwa akipokea euri 18,200 (zaidi ya Sh 38,584). kabla ya kutua KRC Genk, alikuwa akipokea kitita cha dola 15,000 (zaidi ya Sh milioni 32) kutoka kwa TP Mazembe ambayo aliitumia vizuri kujitangaza. Maana yake kwa mshahara atakaokuwa akichukua Samatta inaonekana hakuna tofauti kubwa sana na ule aliokuwa akichukua TP Mazembe. Lakini inawezekana alichoangalia zaidi ni suala la hatua kwa ajili ya kupata mafanikio zaidi hapo baadaye kimshahara pia kiuchezaji kwa ajili ya kutimiza ndoto zake. Kwa mwezi huwa inatajwa kufikia wastani wa euro 20000 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kitanzania. Klabu ya Anderlecht iliyopo nafasi ya tatu katika Ligi, ndio inatajwa kuwa klabu inayolipa mishahara mikubwa zaidi, kwa mwaka Anderlecht inalipa hadi euro 600000 ambazo ni zaidi ya bilioni 1.4 za kitanzania kwa mchezaji mmoja. Klabu ya KRC Genk anayocheza nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta inatajwa kuwa miongoni mwa vilabu tajiri ndani ya Ligi Kuu Ubelgiji, ila kwa mujibu wa www.xpats.com, wachezaji wengi wao Ubelgiji hulipwa kati ya euro 25000 hadi 50000 kwa mwezi. KWa sasa, Samatta ni mwanamichezo anayeshika nafasi ya pili kwa kulipwa mshahara mkubwa nyuma ya Hasheem Thabeet ambaye alikuwa akichukua mshahara hadi dola 200,000 kwa mwezi wakati akikipiga ndani ya NBA na sasa hata kama amepunguziwa kwa kuwa yuko ligi ya chini, haiwezi kuwa chini ya dola 100,000 kwa mwezi
HUU NDIO MSHAHARA ANAOLIPWA MBWANA SAMATTA KATIKA CLUB YAKE MPYA YA KRC GENK
Reviewed by The Choice
on
7:15:00 AM
Rating:
No comments: