BABU TALE AFUNGUKA JUU YA MAGUNGUMZO YANAYO ENDELEA NA KANYE WEST
Meneja
wa Diamond Platnumz amedai kuwa siku msanii wake amekutana na Kanye
West kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa LAX, Marekani, hawakuishia
kupiga picha tu.
Kwanza kutano lao kwa mujibu wa Tale lilikuwa la kama mzaha tu. Anadai kuwa wakati Diamond yupo kwenye uwanja huo alikuja mtu wakati yeye ameinama akimtaka apige picha viatu vyake
Diamond
alishangaa kuona mtu huyo akichukua muda mrefu kupiga picha viatu vyake
na alipoinuka kutaka kumuona, alipata mshtuko wa mwaka kumuona ni
Yeezy.
Ofcourse
lazima upagawe kidogo so baada ya Chibu kubaini kuwa amesimama mbele ya
miongoni mwa rappers wenye ushawishi duniani, anadaiwa kumuimbisha sera
mbili tatu kabla ya kupiga ile picha aliyoiweka Instagram.
“Tuombe
Mungu, tumeweza kupata ukaribu na management yake, kila kitu
kitawezekana, tupo kwenye mazungumzo ya katikati hayajafika mwisho,”
Tale alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.
BABU TALE AFUNGUKA JUU YA MAGUNGUMZO YANAYO ENDELEA NA KANYE WEST
Reviewed by The Choice
on
6:52:00 AM
Rating:
No comments: