Mwanamuziki Diamond na Mtoto wake Tiffah Wapima DNA Sauzi
ISHU ILIKUWA AFRIKA KUSINI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Diamond aliamua kutekeleza mpango huo nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako aliamini hakuna ‘macho mengi’ ya watu, hususan mapaparazi.
SIKIA HII
“Jamani mimi nataka niwape stori ambayo ni ya uhakika. Hivi mnajua kwamba Diamond aliamua kwenda Sauzi kupima DNA yake na mtoto wake Tiffah?
“Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.”
MAJIBU HAYA HAPA
Chanzo hicho kikasema: “Majibu ya DNA yamesema, Nasibu Abdul ni biological father (baba wa damu) wa mtoto Tiffah. Ilibidi jamaa amwage chozi maana alifikiria mengi, watu wamesema sana kuhusu yeye na Tiffah, kwamba si mwanaye, mara ni mtoto wa Ivan (Ssemwanga, mtalaka wa Zari), mara ni mtoto wa pedeshee mmoja wa Bongo. Yaani mengimengi yalisemwa.”
Chanzo: GPL
Mwanamuziki Diamond na Mtoto wake Tiffah Wapima DNA Sauzi
Reviewed by The Choice
on
10:12:00 PM
Rating:
No comments: