Jide Ndoa Tena
Siku chache baada ya kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, mtangazaji
Gardner G. Habash ‘Captain’, mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva anayekuja
na ujio mpya alioubatiza jina la Naamka Tena, Judith Wambura ‘Lady
Jaydee’ au Jide amedaiwa kupata mwanaume mwingine ambaye yupo kwenye
mikakati kabambe ya kumuoa, Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili.
Jide ambaye amekuwa kimya kimuziki kwa zaidi ya miaka miwili, Februari mwaka huu alipewa talaka katika Mahakama ya Manzese-Sinza jijini Dar baada ya mvutano uliodumu kwa muda mrefu tangu wawili hao washindwe kuishi pamoja.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Jide alimpata mwenza muda mrefu tangu walipomwagana na Gardner lakini mipango ya ndoa ikashindwa kwenda haraka kwa sababu hakuwa amepewa talaka hiyo aliyoidai mahakamani.
“Mbona Jide kitambo tu alishapata mtu sema alikuwa hawezi kufanya mambo ya ndoa kwani hakuwa amepewa talaka na Gardner ila sasa hivi yupo huru na mwaka huuhuu huenda kikaeleweka,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Sema Jide kama unavyomjua, mtu wa usiri sana. Anatumia nguvu nyingi kweli kumficha mchumba wake wa sasa. Hataki watu wamjue.”
Mwanahabari wetu alijaribu kumvutia waya Jide kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopatikana aliomba asizungumzie mambo ya uhusiano na badala yake akadai aulizwe kuhusu ujio wake mpya.
“Niulize kuhusu program yangu ya Naamka Tena, nipo bize kuandaa ngoma hiyo na kama unavyoona siku chache zijazo natarajia kuiachia, inanifanya niwe bize sana please niache kwanza,” alisema Jide.
Hata hivyo, mmoja wa mameneja wa msanii huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa kile alichoeleza kuwa hapaswi kumsemea Jide katika masuala ya uhusiano, alikiri Jide kuwa na mchumba ambaye wapo katika hatua nzuri ya kuyaanza maisha ya ndoa.
Chanzo: GPL

Reviewed by The Choice
on
9:51:00 PM
Rating:
No comments: