HIVI NDIVYO RAIS WA VIETNAM ALIVYO POKELEWA AIRPORT YA DAR ES SALAAM JANA USIKU
RAIS
wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Truong Tan Sang, amewasili
nchini jana saa mbili usiku tayari kwa kuanza ziara ya siku tatu
nchini, ambapo pamoja na masuala mengine, atasaini mkataba wa masuala ya
Kodi na mwenyeji wake Rais John Magufuli.
Mkataba huo unalenga kuchochea biashara kati ya Vietnam na Tanzania kwa kuwa utatoa fursa kwa wafanyabiashara wa pande zote kutotozwa kodi mara mbili katika biashara na uwekezaji watakaoufanya.
Rais
huyo anatarajiwa kupigiwa mizinga 21 leo, ikiwa ni pamoja na kukagua
gwaride rasmi, ambapo baadaye atatambulishwa kwa viogozi mbalimbali wa
Serikali, kabla ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa Dar es Salaam kuhusu ujio wa Rais huyo wa
Vietnam, baada ya viongozi hao kutia saini mkataba huo, mgeni huyo na
ujumbe wake atakwenda kwenye ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
iliyopo katika Mtaa wa Lumumba jijini humo kukutana na Mwenyekiti wa
chama hicho, ambaye ni Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Rais
huyo wa Vietnam ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa Chama cha
Kikomunisti cha nchi hiyo chenye uhusiano wa muda mrefu na CCM,
atakwenda kwenye Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) Ubungo,
Dar es Salaam kutembelea viwanda na kupata taarifa za fursa za uwekezaji
katika sekta ya viwanda nchini.
Aidha,
ratiba hiyo imeeleza kuwa atahudhuria mkutano wa biashara na uwekezaji
kati ya nchi hizo mbili, kabla ya kukutana na Spika wa Bunge, Job
Ndungai na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika wakati tofauti.
Pamoja
na ujumbe wake atatembelea hifadhi ya wanyama ya Saadan iliyoko
Bagamoyo na kuondona nchini Machi 11 kuelekea Msumbiji kuendelea na
ziara yake.
Rais
wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe wakishuka
kutoka kwenye ndege mara walipowasili katika Uwanja Ndege wa Kimataifa
wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
(mwenye tai nyekundu) akimkaribisha Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan
Sang (katikati) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius K. Nyerere akiongozana na mkewe 8 Machi, 2016 Jijini Dar es
Salaam.
Rais
wa Vietinam , Trung Tan Sang, Mkewe Mai Thi Hahn na Mkuu, Kassim
Majaliwa wakitazama ngoma baada ya Rais huyo kuwasili kwenye uwanja wa
ndege wa Dar es salam kwa ziara ya siku tatu nchini, Machi8, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
HIVI NDIVYO RAIS WA VIETNAM ALIVYO POKELEWA AIRPORT YA DAR ES SALAAM JANA USIKU
Reviewed by The Choice
on
10:43:00 AM
Rating:
No comments: