Nay wa Mitego Awachukulia R/B Wanaomfuatilia

MKALI wa Bongo Fleva, ambaye wimbo wake wa ‘Shika Adabu Yako’ umefungiwa na Baraza la Sanaa Nchini (Basata), Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’, ameibuka na kudai kwamba ameamua kuchukua R/B kituo kidogo cha polisi ili kuwadhibiti watu anaodai wanamfuatilia kwa nia ya kumtendea mabaya.
nay987
“Kiukweli sina ugomvi na mtu na hii ni dunia haina siri, kama kuna mtu ananifanyia hivyo vitu basi itajulikana maana mimi nimeimba kama wimbo mwingine na sina ugonvi nao, sasa kama wananitafuta nitawatafuta kwa R/B,” alieleza.
Aliongeza kwamba, kwa sasa mtoto wake wa kike amefanyiwa upasuaji wa uvimbe katika koo na maendeleo yake ni mazuri, huku akisisitiza kwamba Ijumaa ya wiki hii atatoa video ya wimbo wake huo.
“Mwanangu alikuwa anaumwa lakini kwa sasa nashukuru Mungu hajambo na wiki hii nitatoa video ya wimbo wangu, mtaona tofauti na mnavyofikiria tofauti katika wimbo wenyewe,’’ alimaliza
Mtanzania
Nay wa Mitego Awachukulia R/B Wanaomfuatilia Nay wa Mitego Awachukulia R/B Wanaomfuatilia Reviewed by The Choice on 8:46:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.