Watu Wanne Watiwa Mbaroni Sengerema Kwa Kunywa Pombe Mchana
Wilaya
ya Sengerema imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais baada ya
kukamata watu wanane waliokutwa wakinywa pombe saa za kazi.
Amri
ya kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa watu hao ilitolewa juzi na Mkuu wa
Wilaya Zainabu Terack baada ya kukuta baa zimefunguliwa asubuhi zikiwa
na wateja waliokuwa wakipata kinywaji kabla ya saa 9:30 alasiri, muda
ambao ofisi za Serikali hufungwa.
Rais
John Magufuli alitoa agizo hilo la kupiga marufuku unywaji pombe na
uchezaji pool nyakati za kazi wakati alipokuwa akiwaapisha wakuu wa
mikoa mwezi uliopita. Alitaka vijana ambao watakaidi maelezo ya
kuambiwa, nguvu itumike kuwalazimisha kufanya kazi.
Kwa
mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, aliyeongoza oparesheni ya dakika 45 ya
kusaka wanaokunywa pombe na kucheza pool muda wa kazi, watuhumiwa hao
watafikishwa mahakamani kwa makosa ya uzembe na kukiuka amri halali ya
serikali.
Wakijitetea
baada ya kutiwa mbaroni, baadhi ya waliokamatwa walidai kuwa walienda
baa kujiliwaza wakati wa msiba wa ndugu yao waliyemtaja kwa jina la
Petro Shoyo, na kumwomba mkuu wa wilaya kuwasamehe kwa sababu ni kosa
lao la kwanza.
Watu Wanne Watiwa Mbaroni Sengerema Kwa Kunywa Pombe Mchana
Reviewed by The Choice
on
7:46:00 PM
Rating:
No comments: