SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAWEKA REKODI KATIKA USHIRIKI WA MATEMBEZI YA HISANI.

 
Bw. Jeyapaulraj, akipokea nyaraka kwa niaba ya Abu Dhabi Indian School, mshindi wa shule na kituo cha kikundi cha watoto yatima.

Bibi Atija, akipokea nyara kwa niaba ya Mkuu wa Umoja wa Wanawake, mshindi wa kikundi cha wazee.

Bi Linda Celestino, Makamu wa Rais huduma za wageni shirika la Etihad, akipokea nyara kwa niaba ya wizara, mshindi wa Makampuni na kikundi cha Vilabu.

Mtoto akichunguza mashine ya mazoezi ya kupaa na marubani Etihad Airways.

Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Etihad wakiwa na watoto katika bustani ya  Al Mushrif

Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Etihad wakiwa na umati wa watu.

Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Etihad, Wahudumu wa watoto, marubani, Ali Al Shamsi, Makamu Rais wa mikakati akiwa na watoto wenye Autism.

Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Etihad wakiwa na watoto katika bustani ya  Al Mushrif

Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Etihad na timu ya Alitalia

Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Etihad na marubani wakiwa na watoto.

Chini ya ulezi wake Mtukufu, Sheikha Shamsa bint Hamdan Bin Mohamed Al Nahyan, Mheshimiwa mwenyekiti wa kituo cha Autism mjini Abu Dhabi, Shirika la ndege la Etihad limeendesha hafla hiyo ya kuchangisha fedha kwa sababu maalum kupitia matembezi.

Zaidi ya washiriki 5,200 wa kila umri walikusanyika katika bustani za Al Mushrif Central  Mjini Abu Dhabi siku ya Ijumaa Machi 18 kushiriki katika tukio la matembezi ya dakika  30.

Fedha zote zilizotolewa katika tukio zitakwenda katika ujenzi wa jengo jipya litalokuwa kituo kipya cha utabibu mjini Abu Dhabi kwa ajili ya waathirika wa ugonjwa wa Autism, pamoja na ukarabati wa shule nchini India.

Mtukufu Sheikha Shamsa bint Hamdan Bin Mohamed Al Nahyan alitoa pongezi kwenda shirika la ndege la Etihad kwa ajili ya maandalizi ya tukio hilo, ambayo inaonyesha dhaira ya kampuni kuendelea kusaidia kuleta maendeleo ya kijamii na uboreshaji endelevu katika jamii zinazo wazunguka .

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Mtukufu Sheikh Thiyab Bin Khalifa Bin Hamdan Al Nahyan, Eugenia Davis, Baraza la Umoja wa Mataifa ya Amerika, Kanali Abdulrahman Al Swaidi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Shayma Nawaf Fawwaz, Afisa Mtendaji Mkuu wa GOSSIP, Mheshimiwa Mariem Al Rumaithi, Mjumbe wa Bodi ya Shirika la matunzo ya kibinadamu na Mahitaji Maalum la Zayed , na Dk. Khawla Salem Rashed Al Saaedi, mwakilishi wa Rais wa Wanawake na Health Alliance International.

Khaled Al Mehairbi, Makamu wa Rais wa uendeshaji wa uwanja wa ndege wa Abu Dhabi na Mwenyekiti wa Michezo na kamati za kijamii katika shirika la ndege Etihad, alisema: "Shirika la ndege Etihad lina nia ya kutoa huduma bora kwa watoto wenye ugonjwa wa akili ili kuboresha ubora wa maisha yao.

"Hii ni sehemu ya ahadi yetu kuendelea kuleta maendeleo kwa jamii yetu ya ndani na kuboresha afya ya umma na kuongeza ufahamu wa autism.”

"Matembezi haya ya faraja kwa mara nyingine tena imewaleta kwa pamoja jamii ya Abu Dhabi, na tuna matumaini kuwa na uwezo wa kuongeza ufahamu na fedha muhimu kwa kusaidia watu wenye mahitaji – hapa nyumbani pamoja na kimataifa”

Matebezi hayo yalikuwa wazi kushiriki kwa watu wa miaka yote, baada ya usajili washiriki walipokea kipima spidi pamoha na fulana iliyobeba nembo ya tukio hilo.

Bibi Athba Ali, meneja manunuzi wa shirika la ndege la Etihad  na mama wa watoto wawili, alisema: "Mimi nina furaha na fahari kuwa sehemu ya tukio hili la “Tembea kwa Hisani" tukio hilo. Nina furaha kuona kwamba tukio limefanikiwa katika kuleta kila mtu pamoja ili kusaidia kufanikisha tukio hili. Tulifurahia tukio hili la matembezi na tayari tunatazamia tukio la mwaka ujao.”

Burudani kutoka “Bollywood” ilikuwepo kuwapa washiriki motisha na burudani huku shirika la ndege la Etihad waliandaa shughuli mbali mbali kwa ajili ya wanafamilia wote ikiwa ni pamoja na mazoezi ya kurusha ndege chini ya nahodha wa ndege pamoja na warsha ya mapishi ya ndani ya ndege chini ya mpishi mkuu.  Wahudumu wa watoto walikuwepo kusaidia kusimamia na kuchangamsha watoto.

Wakati wa mchezo wa 'Jaribu na ushinde', waliohudhuria walikuwa na nafasi ya kushinda idadi kubwa ya zawadi ikiwa ni pamoja na tiketi daraja la uchumi kutoka shirika la ndege la Etihad, Bidhaa zisizolipiwa ushuru za bure, Uanachama wa mwaka mmoja kwa famila nzima wa Kituo cha kimataifa cha mapumziko na michezo cha Al Forsan, malazi ya wikiendi nzima katika hoteli ya nyota 5, Vocha ya watu wawili ya mlo wa usiku, zawadi kutoka kwa Apparel Group na mengi zaidi.

Wadhamini wa tukio la mwaka huu walikuwa: Wizara ya Mambo ya Ndani, Jamii ya Autism Emirates, Abu Dhabi Media Company, Emirates Red Crescent, Baraza la elimu la Abu Dhabi, Braza la michezo la  Abu Dhabi, Kampuni ya maji ya Al Ain, Bustani ya Mushrif, Shirika la Zayed, Verde, Austin Reed, Glossip Milano, Muungano wa wanawake wa Hindi, Gossip Café na Desserts, Canon Mashariki ya Kati, wa Kituo cha kimataifa cha mapumziko na michezo cha Al Forsan, Hospitali ya LLH, Nyumba ya sanaa ya kisasa Etihad, Kampuni ya uchapishaji ya United, Silkor, Primavera Medical Rehabilitation LLC, Crowne Plaza na Staybridge Suites Abu Dhabi Yas Island, Holiday Inn Abu Dhabi, Rosewood Abu Dhabi, Hoteli ya Royal Rose, Landmark Gulf Group, Kituo cha marekani cha vipaji maalum, Kituo cha tiba ya meno cha Boston na Mercure Al Ain Grand Jebel Hafeet.
***MWISHO***

Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na  airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com
SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAWEKA REKODI KATIKA USHIRIKI WA MATEMBEZI YA HISANI. SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAWEKA REKODI KATIKA USHIRIKI WA MATEMBEZI YA HISANI. Reviewed by The Choice on 7:37:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.