RAIS NA AFISA MKUU WA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD AHUTUBIA KONGAMANO LA HUDUMA ZA MIZIGO LILOFANYIKA JIJINI ABU DHABI
James Hogan - PCEO Etihad Airways |
Rais na afisa mkuu wa shirika la ndege la Etihad,
bwana James Hogan alitoa hotuba ya ufunguzi mbele ya zaidi ya wajumbe 1,200 waliohudhuria
kongamano kuu la masuala ya huduma ya mizigo lilofanyika katika kituo cha maoneyesho
cha Abu Dhabi kuanzia tarehe 10 hadi 13 Machi.
Bwana Hogan aliongelea kiundani juu ya
mabadiliko katika sekta ya mizigo na jinsi gani muungano wa washirika wa shirika
la ndege la Etihad umeongeza nguvu katika utendaji kazi wa kitengo hicho cha
mizigo. Kwa kuunganisha ndege za mizigo na mitandao yake, kitengo cha mizigo
cha Etihad kinatambulika kama kitengo namba tano (5) kwa ukubwa duniani kikishirikiana
kwa ukaribu wa dhati na kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Jet, kitengo
cha mizigo cha shirirka la ndege la berlin, Serbia, Alitalia, na kitengo cha
mizigo cha shirika la ndege la Seychelles.
Kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Etihad
hutengeneza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani kama mapato ya mwaka na kukifanya
kuwa moja ya kitengo cha mizigo chenye
mafanikio zaidi duniani. Kilifanikiwa
kuhudumia asilimia 88 ya mizigo yote iliyoingia, iliyotoka na iliyosafirishwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi
mwaka 2015, mwaka ambao kitengo hicho kilibeba tani 529,090 za mizigo na barua,
jumla ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 4 ya mwaka 2014.
Kwa sasa kitengo cha mizigo cha Etihad kwa
kutumia ndege nne aina ya boeing 777F, tatu aina ya boeing 747s, na nne aina ya
airbus A330s. ndege iliyoongezwa aina ya boeing 777 inatazamiwa
kuwasili ndani ya mwezi huu uku nyingine aina ya airbus A330 ikiwa imepangwa
kuwasili mwaka 2017.
Bwana Hogan alizungumzia
jinsi gani Kanda ya Mashariki inaendelea kufanya vizuri katika viwango vya ukuaji
wa kimataifa kwenye sekta ya mizigo na ina jukumu muhimu katika mtiririko wa
biashara na bidhaa duniani, pamoja na umuhimu wake wa kijiografia kuimarika
kutokana na wadau kuhama masoko ya zamani yaliojazana na kuanzisha masoko mapya
katika vituo vya biashara huko Mashariki ya Kati, Asia, Amerika ya Kusini na
Afrika.
Alisema: "Kitovu
chetu cha Abu Dhabi ni njia panda ya dunia chenye kitengo kikubwa cha
kushugulikia mizigo, Shirika la ndege la Etihad limejiweka nafasi
nzuri kunufaika na ongezeko la abiria, ongezeko la mizigo na bidhaa
zinazosafirishwa baina ya masoko makubwa na yale mapya”
Etihad Cargo inatoa
huduma ya kubeba mizigo kawaida ndani ya ndege pamoja na kwenye buti la ndege
huduma hizi zikifikia mtandao wa abiria pamoja na vituo vya mizigo tu.
"Kitengo cha mizigo
cha Etihad kimekuwa biashara inayoingiza mapato ya mabilioni na inawakilisha
sehemu kubwa ya biashara yetu kwa kujidhatiti kutoa huduma maalumu kwa wateja
pamoja na bidhaa zenye ubunifu zenye kutoa ushindani mkubwa na kuvutia wateja
wetu. Kwa kufanya kazi na washirika wetu, tutaendelea kuongeza faida ya kila kituo
cha mizigo kwa kuchanganya rasilimali, mitandao na uwezo kwa manufaa ya wateja
wetu wote "alisema Bw Hogan.
RAIS NA AFISA MKUU WA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD AHUTUBIA KONGAMANO LA HUDUMA ZA MIZIGO LILOFANYIKA JIJINI ABU DHABI
Reviewed by The Choice
on
2:09:00 PM
Rating:
No comments: